Amiri
Jeshi Mkuu, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Joseph Magufuli akisalimiana na wananchi wa Arusha Mjini wakati akipita
kuelekea Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi (TMA) Monduli ambako pamoja na
mambo mengine kesho tarehe 23 Januari, anatarajiwa kutunuku Kamisheni
kwa Maafisa wanafunzi wa Chuo cha Mafunzo ya Kijeshi Monduli kundi la
57/15.
Amiri
Jeshi Mkuu,Rais Dkt Magufuli akiwasikiliza wananchi kwa makini
alipopita maeneno ya Sanawali kuwasalimia wakati akielekea Wilayani
Monduli.
Baadhi
ya Wananchi wa Maeneo ya Sanawali wakishangilia ujio wa Rais John Pombe
Joseph Magufuli,alipokuwa akielekea Wilayani Monduli mapema leo
asubuhi.
Rais
Magufuli akiwa amevalia sare za kijeshi amesimamishwa na kuwasalimu
wananchi katika maeneo ya SANAWALI, TEKNIKO, NGARENALO, MBAUDA, MAJENGO
na KISONGO
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
akisalimiana na wananchi wa Kisongo nje kidogo ya jiji la Arusha waliojitokeza
kumsalimia wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Mbauda Mkoani Arusha hawaonekani
pichani wakati akielekea Monduli kwa ajili ya kufunga zoezi la Onesha uwezo
Medani.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akisoma bango alilokabidhiwa na mwananchi mmoja
katika eneo la Kona ya Nairobi Mkoani Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akiwahutubia wananchi wa Arusha katika eneo karibu na chuo cha Arusha Tech.
Wananchi hao walifunga barabara ili wapate nafasi ya kumuona Mheshimiwa Rais
Dkt. Magufuli
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akihutubia wananchi wa Mianzini Mkoani Arusha.
Umati mkubwa uliojitokeza katika eneo la Mianzini Mkoani
Arusha
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General
Davis Mwamunyange wakati waufungaji wa zoezi la Onesha Uwezo Medani
lililofanyika Monduli nje kidogo ya Jiji la Arusha.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akijadiliana jambo na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Nchini General Davis
Mwamunyange wakati akielekea kupewa maelezo ya zoezi zima la Onesha Uwezo
Medan.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya Maafisa wa jeshi katika tukio hilo la
Ufungaji.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli
akielekea kwenye uwanja wa maonesho akiwa pamoja na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi
Nchini General Davis Mwamunyange.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Waziri wa Ulinzi na Jeshi la
Kujenga Taifa Dkt Hussein Mwinyi, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni
Sefue, Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Daudi Ntibenda, Mkuu wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange na Maafisa wa ngazi za juu wa Jeshi mara
baada ya kufunga zoezi la Onesha Uwezo Medani Monduli Mkoani Arusha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John
Pombe Magufuli katikati akishuhudia matukio ya zoezi la Onesha Uwezo Medani
Monduli Mkoani Arusha.
SHARE
No comments:
Post a Comment