TRA

TRA

Wednesday, March 29, 2017

Ufaransa na Indonesia waahidi kutia msukumo kufikia amani ya Mashariki ya Kati

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
UFARANSA na Indonesia zimekubaliana kufanya juhudi zote kutafuta amani kati ya Wapaletisna na Israel.

Hayo ameyasema rais wa Indonesia Joko Widodo.Rais wa Ufaransa Francois Hollande amefanya mazungumzo na mwenzake wa Jarkata Joko Widodo mjini Jakarta ikiwa ni ziara ya kwanza ya kiserikali ya rais wa Ufaransa nchini Indonesia katika kipindi cha miaka 30.

Hollande amesema kwamba suala la uhuru wa Palestina na mapambano dhidi ya itikadi kali na ugaidi ni mambo waliyojadiliana na mwenzake katika ikulu ya mjini Jarkata.

Aidha rais Joko Widodo amefahamisha kwamba wamekubaliana pamoja na Ufaransa kuendeleza juhudi za kupatikana amani kati ya Israel na Palestina kupitia mpango wa kuundwa madola mawili na kuongeza kwamba ni muhimu kuunga mkono hali ya kuvumiliana na kukabiliana na ubaguzi ili kuzima harakati za itikadi kali.

Ziara ya Hollande Indonesia ni sehemu ya safari yake katika ukanda wa Kusini Mashariki ambayo imemfikisha pia Singapore na Malysia.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger