Mkurugenzi
Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi
na maendeleo ya Makazi, George Pangawe akizungumza na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam leo kuhusiana na Zoezi la bomoa bomoa
linaliendelea katika kingo za mto Msimbazi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mkurugenzi
Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji miji Wizara ya Ardhi
na maendeleo ya Makazi, George Pangawe jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Emmanuel Massaka wa Globu ya Jamii.
Na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SERIKALI
yawaomba wananchi waliojenga makazi kwenye sehemu hatarishi, kingo za
mito na maeneo ya wazi kuhama kwa hiyari yao ili kupisha Oparesheni ya
bomoa bomoa kuendelea bila kikwazo.
Hayo
yamesemwa na Mkurugenzi Msaidizi wa usimamizi na udhibiti wa uendelezaji
miji Wizara ya Ardhi na maendeleo ya Makazi, George Pangawe wakati
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Pangawe
amesema kuwa Serikali itahakikisha haki inatendeka kwa wananchi wote
pia itahakikisha haki na usawa wa pande zote wakati wa utekelezaji wa
zoezi la bomoabomoa linaloendelea tangu lilipoaza tena Januari 5 mwaka
huu.
Zoezi
la bomoabomoa linaendelea jijini Dar es Salaam katika kingo za mto
Msimbazi ili kuepusha wananchi kupatwa na madhara mbalimbali ambayo huwa
yanakitokeza wakati wa mvua kubwa na masika.
Pangawe
pia amesema kuwa bonde la mto msimbazi liliainishwa kama ni sehemu
hatarishi kwa makazi ya binadamu tangu 1979 na wananchi wa maeneo ya mto
huo wakaanza kuvamia kutokana uhaba wa maeneo ya makazi na kuanza
kujenga katika kingo za mto huo.
Pia
amewasihi wananchi kutii sheria za ardhi bila shuruti ili kuepukana na
madhara mbalimbali yanayojitokeza pamoja na upotevu wa mali zao.
SHARE
No comments:
Post a Comment