Tangazo kuhusiana na jaribio hilo la bomu la Hydrogen la Korea Kaskazini
Siku moja
baada ya Korea Kaskazini kufanya jaribio la bomu la nyuklia aina ya
Hydrogen, Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limekubaliana kuanza
mikakati ya kuiwekea vikwazo kufuatia jaribio hilo.
Hata
hivyo baadhi ya Wataalam wameonyesha kuwa na wasi wasi kuhusu jaribio la
sasa la Nyuklia la Korea Kaskazini ambalo ni la nne katika muongo mmoja
kwamba nguvu yake inaweza kuwa ni bomu la hydrogen.
Kwa faida
yako tu bomu la hydrogen ni moja ya mabomu hatari ya jamii atomic au
nyuklia yenye nguvu zaidi. Wataalam wanasema bomu hili la hydrogen lina
uwezo mkubwa kiasi kwamba linaweza kulipua mji mmoja wote kwa mlipuko
mmoja.
Kufuatia
jaribio hilo jamii ya kimataifa imendelea kulaani tukio hilo Katibu Mkuu
wa Umoja wa Mataifa ambaye pia ni Waziri wa zamani wa Mambo ya nje ya
Korea Kusini Ban Ki moon yeye amesema jaribio hilo la bomu la nyuklia ni
hatua ya kuogopesha.
"Hili
jaribio kwa mara nyingine limekiuka maazimio kadhaa ya Baraza la Usalama
la Umoja wa Mataifa pamoja na wito wa pamoja wa Jamii ya kimataifa
kukomesha vitendo hivyo. Pia linakwenda kinyume kabisa na utamaduni wa
kimataifa wa majaribio ya mabomu ya nuclear. Tendo hilo linaonekana ni
la kuogopesha kwa usalama wa kanda na kupuuza juhudi za kimataifa za
kuacha kutengeza. Ninalaani kwa nguvu jambo hilo."
Huko
Marekani nayo Ikulu ya White house imesema utafiti wake wa awali kuhusu
jaribio hilo la bomu nyuklia la Korea ya Kaskazini haufanani na madai
kwamba nchi hiyo imefanikiwa kulipua bomu la Hydrogen.
Msemaji
wa White house Josh Earnest amesema kutengwa kwa Korea ya Kaskazini
unapaswa kuimarishwa zaidi kama itaendelea na matendo yake ya ukiukaji
ikiwa ni pamoja na kufanya majaribio ya makombora ya angani.
"Tumesikitishwa
sana na matokeo ya uharibifu wa amani na utulivu baada ya matendo ya
ukiukaji wa Korea Kaskazini kuzidi kuongezeka. China na Urusi nao pia
wamesikitishwa . Ndio maana tunafanya bidii kuiweka pamoja jamii ya
kimataifa na kuweka wazi kwa Korea Kaskazini kwamba njia ni moja tu
iliyobaki ambayo ni nzuri kwa raia wa Korea Kaskazini, ambayo itakuwa
nzuri kwa uchumi wa Korea kaskazini, nzuri kwa nchi Korea kaskani kwa
maana ya uwezo wao wa kujihusisha na jamii ya kimataifa."BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment