ETIHAD imetunukiwa tuzo ya kifahari ya “Uvumbuzi katika Usafiri”
katika hafla iliyoandaliwa na jarida la Travel Weekly ya kuwatunza wadau
wa sekta ya usafiri dunia nzima huko Uingereza maarufu kama “Globe
Travel Awards”. Hafla hiyo ilifanyika katikati ya wiki kwenye hoteli
maarufu ya Grosvenor House, iliyopo Jijini London.
Kwa kawaida tuzo hii hupewa kampuni ambayo imevumbua bidhaa au
huduma yenye kuleta wimbi la mabadiliko na maendeleo katika soko.
Shirika la Etihad waliibuka washindi baada ya jopo la wataalamu kuamua
kwamba Shirika linastahili tuzo hii kutokana na huduma yake ya “Makazi”-
ambayo ni huduma binafsi ya kipekee duniani yenye kutoa vyumba vitatu
kwenye ndege ya Etihad. Huduma hii, iliyoleta mapinduzi katika sekta ya
usafiri wa anga,ni matokeo ya programu ya utafiti na maendeleo
iliyoendeshwa kwa miaka saba na kusimamiwa na timu nzima ya ubunifu
kutoka kituo cha Uvumbuzi, Jijini Abu Dhabi.
“Makazi” yanayopatikana kwenye ndege za Etihad aina ya Airbus A380
yana ukubwa wa mita za mraba 11 na ndani yake kuna sebule, bafu la
pembeni, chumba kikubwa cha kulala na mhudumu mmoja kwa kila chumba.
Shane O’Hare, Makamu Rais wa Masoko wa Shirika la ndege la Etihad
alisema: “Tunafurahishwa na uamuzi wa jopo la wataalamu wa tuzo za Globe
Travel, ambao ndio walipiga kura ‘Makazi’ kuwa huduma bora
iliyovumbuliwa katika sekta yetu. Vyumba hivi vimebadili mitazamo ya
wengi, vikiwapa fursa watu wa kawaida kufurahia huduma zinazopatikana
mara nyingi katika ndege binafsi tu.”
“Etihad inathamini ushirikiano kati yake na soko la Uingereza,
uhusiano ulioanza tulipozindua safari zetu kuelekea na kutoka uwanja wa
ndege wa Heathrow uliopo jijini London mnamo mwaka 2004. Tumeinua hadhi
ya usafiri ikiwa ni pamoja na kuzipa ndege zetu muonekano halisia wa
makazi ya kuishi na kuwapa wasafiri viwango vya hali ya juu vya faragha
na utulivu”.
Huduma ya ‘Makazi’ inapatikana ndani ya ndege aina ya A380
zinazofanya safari zake kati ya Abu Dhabi na London, New York pamoja na
Sydney. SHirika la Etihad linatazamia kuzindua huduma hii katika ndege
ziendazo Mumbai na Melbourne mwaka huu.
Etihad ina timu maalumu ambayo kazi yake pekee ni kuhakikisha
wanaochagua kusafiri na ndege zao wanaweza kufuruahia vyumba ya ‘Makazi’
wapendavyo. Timu hii pia ipo karibu na watoa huduma maalum waliopo
kwenye vyumba hivi. Wateja wanapewa fursa ya kufurahia huduma mbalimbali
wakiwa wanasafiri na ndege hii ya Etihad zikiwemo; kuweka oda ya mahala
pa kula, burudani ndani ya ndege, matukio maalum kama sherehe za
kuzaliwa, maelezo kuhusu waendako na kadhalika. Watuapo, timu hiyo
maalum (VIP) huwasaidia wageni katika kufanya taratibu za kuwasili na
usalama.
Ndege za Etihad zinafanya safari zake kwenda Uingereza kutwa mara
sita, pamoja na kutoa huduma za safari za moja kwa moja kati ya uwanja
wa ndege wa Heathrow uliopo jijini London na kuelekea Machester na
Ediburgh, zilizoanzishwa Juni 8 mwaka jana. Uwanja wa ndege wa Heathrow
ulipewa nafasi kuwa kiwanja cha kwanza ndege aina ya Airbus A380 za
Etihad kutua kwa mara ya kwanza, na hivyo huduma hiyo ilianza mwishoni
mwa mwaka 2014.
SHARE
No comments:
Post a Comment