Mkurugenzi
Mkuu wa Bayport Financial Services, John Mbaga, kulia akizungumza jambo
katika uzinduzi wa huduma mpya wa mikopo ya viwanja vinavyotolewa na
taasisi yao katika maeneo sita ambayo ni Kilwa, Bagamoyo, Kigamboni,
Chalinze, Kibaha na Morogoro. Kulia kwake ni Zahra Moore kutoka kwenye
kampuni yao ya BlackWood na Mwanasheria wao Ntiiba Muganga. Picha na
Story kwa Hisani ya Bayport Financial Services.
TAASISI
ya Kifedha ya Bayport Financial Services inayojihusisha na mikopo,
imezindua miradi sita mipya ya mikopo ya viwanja katika maeneo ya
Kibaha, Bagamoyo, Chalinze, Temeke, Kilwa na Morogoro, ikiwa ni
mwendelezo wa utoaji huduma bora za viwanja baada ya ule wa Vikuruti
kuungwa mkono Watanzania wengi.
Kuzinduliwa
kwa huduma hizo mpya za viwanja huku wakiongozwa na Mbunge wa
Kigamboni, Faustine Ndugulile, mwakilishi wa Mkuu wa Wilaya Temeke,
Martha Minga, kunatanua wigo wa urahisishaji wa maisha ya Watanzania,
hususan katika suala la ardhi linalozidi kupanda thamani siku hadi siku,
jambo linalohitaji juhudi za taasisi kama Bayport za kuwasaidia
wananchi wake kupata maeneo ya makazi kwa utaratibu rahisi na nafuu.
Mwakilishi
wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga, aliyesimama akizungumza
katika uzinduzi wa hudumaya viwanja inayotolewa na taasisi ya kifedha ya
Bayport Financial Services, leo mchana katika Ukumbi wa Ramada Encore,
Posta, jijini Dar es Salaam. Anayeshuhudia ni mwanasheria wa Kampuni ya
BlackWood, Ntiiba Muganga na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa BlackWood Zahra
Moore.
Akizungumza
katika uzinduzi wa miradi hiyo mipya ya viwanja, Mkurugenzi Mkuu
Bayport Financial Services, John Mbaha, alisema huduma zao zitakuwa na
njia rahisi kwa ajili ya kuwawezesha wananchi wote kuchangamkia fursa ya
upatikanaji wa viwanja hivyo.
Meneja
Masoko na Mawasilianowa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo kushoto
akibadilishana mawazo na Mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha
Minga.
Mkurugenzi
Mkuu wa Bayport Financial Services, Jonh Mbaga, akipiga picha ya pamoja
na Mbunge wa Kigamboni, Mheshimiwa Faustine Ndugulile katika uzinduzi
wa huduma ya mikopo ya viwanja, uliofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Kushoto ni mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Bi Martha Minga.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo
akizungumza katika uzinduzi huo wa huduma ya mikopo ya viwanja.
Meneja
Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, akimsikiliza kwa
makini Mkurugenzi Mkuu wa taasisi yao John Mbaga kulia kwake wakati
anazungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi wa huduma yao ya mikopo
ya viwanja.
Alisema
njia hizo ni pamoja na ununuaji wa kiwanja kwa pesa taslimu ambapo
mteja anatakiwa kulipia fedha zote za kiwanja kwenye akaunti ya Bayport,
kukabidhi nakala za nyaraka za malipo hayo kwenye ofisi za Bayport na
kusubiri ndani ya siku 90 ili akabidhiwe hati yake baada ya kukamilisha
malipo yote.
“Kwa
wateja wa mkopo wa upande wa ujasiriamali na watumishi wa kampuni
binafsi, wanatakiwa kulipia malipo ya awali ya mita za mraba
walizochagua, huku Bayport ikikamilisha malipo yaliyosalia na wateja hao
kupatiwa nyaraka zao baada ya kukamilisha mkopo wao, ambapo thamani ya
viwanja hivyo vikianzia sh Sh 550,000,” Alisema Mbaga.
Naye
Meneja Biashara wa Bayport Financial Services, Thabit Mndeme, alisema
watumishi wa umma hawatakuwa na gharama za awali, badala yake wakichagua
maeneo watakayo, wataingizwa kwenye kundi la mkopo na kutakiwa kulipa
mkopo huo kila mwezi kwa kipindi cha miaka mitatu, huku makato
yakikadiliwa kuwa Sh 73,684.49 kila mwezi.
“Bado
tunaendelea kutanua wigo kwa watu wote kama vile watumishi wa umma,
watumishi wa kampuni binafsi, bila kusahau kundi kubwa la wajasiriamali
ambalo limeendelea kujumuishwa kwenye miradi yetu ya viwanja, tukiamini
gharama ya makato ya kila mwezi ya Sh 102,855 ni rahisi na yanaweza kuwa
mkombozi wa maisha ya watu wengi,” alisema Mndeme.
Kwa
mujibu wa Mndeme, huduma za viwanja zinapatikana katika maeneo ya
Bagamoyo na mita moja za mraba zitauzwa kwa Sh 10,000 tu na (Boko
Timiza) Kibaha mita moja za mraba itauzwa kwa Sh 9,000 na (Kibiki na
Mpera) Chalinze mita moja za mraba zitauzwa Sh 4500, huku (Tundi
Songani) Kigamboni mita moja ya mraba itanunuliwa kwa Sh 10,000 na
(Msakasa) Kilwa mita ya mraba itapatikana kwa Sh 2000, bila kusahau
(Kiegea) mita moja ya mraba Sh 3500 tu.
Naye
Meneja Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
alisema kwamba hakuna Mtanzania atakayelalamika kushindwa kujenga
nyuumba, kama watafanyia kazi juhudi za taasisi yao yenye dhamira na
malengo makubwa ya kuwakwamua watu wote ili wawe na vitu vya thamani
kama vile nyumba na viwanja.
Kwa
upande serikali kwa kupitia mwakilishi wa Mkuu wa wilaya Temeke, Martha
Minga, aliitaka Bayport kushirikiana na serikali katika mambo yao
hususan ya viwanja ili kuhakikisha kwamba wananchi wanafanikiwa kwa
dhati na kuepusha migogoro hususan katika suala zima la hati ambalo ndio
muhimu katika mambo yanayohusiana na ardhi.
Naye
Mbunge wa Kigamboni Faustine Ndugulile alisema kwamba amefurahishwa mno
na huduma ya viwanja vya Bayport sambamba na kuguswa kwa jimbo lake la
Kigamboni, jambo linaloweza kuiweka eneo hilo katika nafasi za juu.
Mkurugenzi
wa Uzalishaji wa Kampuni ya BlackWood Zahra Moore kushoto akizungumza
jambo katika uzinduzi wa huduma ya viwanja ya Bayport Financial
Services.
Mwanasheria wa Kampuni ya BlackWood Ntiiba Mungana akizungumza jambo kwenye uzinduzi huo wa huduma ya mikopo ya viwanja.
Meneja
Masoko na Mawasiliano wa Bayport Financial Services, Ngula Cheyo,
akipiga picha ya pamoja na Mkurugenzi wa Uzalishaji wa kampuni ya
BlackWood, Bi Zahra Moore
SHARE
No comments:
Post a Comment