TRA

TRA

Monday, February 22, 2016

Sweden Yaipongeza Tanzania, Benki ya CRDB

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !
Afisa uendeshaji wa Benki ya CRDB Microfinance,  Samson Keenja,  akielekeza utoaji huduma za kifedha vijijini kwa Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Sweden, Kenneth Forslund, aliyeongoza ziara ya Wabunge wa Sweden.


Sweden imeipongeza Tanzania, katika juhudi zake zake kuhakikisha huduma za kifedha zinasambazwa nchi nzima hadi maeneo ya vijijini, ambapo hayafikiwi na huduma za kifedha, kufuatia huduma za kifedha zinazotolewa na benki ya CRDB, Fahari Huduma, ambazo zimesambaa katika vijiji vyote, hivyo kulifanya taifa la Tanzania kuongoza katika nchi za Afrika ya Mashariki kufikisha huduma za kifedha katika maeneo mengi ya vijijini.

Pongezi hizo, zimetolewa na Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje wa Bunge la Sweden, Bw. Kenneth Forslund, aliyeongoza ziara ya Wabunge wa Sweden, kukagua shughuli mbalimbali za maendeleo zinazofadhiliwa na serikali ya Sweden.  Mhe. Forslund, ameisifia Tanzania, kwa jinsi Tanzania inavyotumia vizuri misaada ya kimaendeleo ya Sweden, katika kutimiza malengo yaliyokusudiwa, ambapo moja ya taasisi zilizofadhiliwa na Sweden, ni FSDT inayoifadhili benki ya CRDB, kusambaza huduma za kibenki za Fahari Huduma.

Afisa uendeshaji wa Benki ya CRDB Microfinance,  Samson Keenja, amesema baada ya CRDB  kugundua kuwa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania, umewafikia wananchi wachache sana tena wa mijini tuu,  ndipo Benki ya CRDB,  kwa kushirikiana na Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha (FSDT)  wakaanzisha Wakala wa Huduma za Kifedha, (Agents Banking) na CRDB kuanzisha huduma ya Fahari Huduma ambapo mawakala wa Fahari Huduma wametapakaa mpaka vijijini, hivyo kusogeza huduma za kifedha karibu na wananchi.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Kuendeleza Sekta ya Fedha nchini FSDT, Bw. Sostenes Kewe, amesema mfuko wake unalenga katika kupanua wigo upatikanaji wa huduma za kifedha kuwafikia watu wengi zaidi, ambapo wameshirikiana na benki ya CRDB katika usambazaji wa huduma hizi. Amesema huduma za kifedha ni muhimu sana katika kuendesha maisha ya wananchi, ni muhimu katika ukuzaji na uendelezaji biashara ndogondogo na za kati, katika ukuaji wa uchumi, utengenezaji ajira na upunguzaji umasikini.

Wajasiliamali Mainda Mwakalinga na mumewe, Frank Mwakalinga ambao ni waendeshaji wakala wa Fahari Huduma eneo la Kibamba, wameishukuru benki ya CRDB kuwasogezea huduma za kifedha karibu na maeneo yao, kwa sababu kabla ya hapo, watu wa Kibamba walilazimika kusafiri hadi Mbezi Mwisho au Kibaha kupata huduma za kifedha lakini sasa CRDB imewaletea huduma mpaka mlangoni.

Naemjasilamali mdogo, Bi Janet Tomaslisha, anayefanya biashara ndogo ndogo, aliishukuru CRDB kwa kuwasogezea huduma za kifedha na kuwapatia mikopo midogo midogo ya ujasiliamali bila dhamana, aqkasema mikopo hiyo ni midogo mno, hivyo kuwaingizia kipato cha kuendesha tuu maisha yao, lakini akaiomba benki ya CRDB kuwapatia mikopo mikubwa wajasiliamali wadogo wadogo ili waweze kukua na kufanya biashara kubwa kubwa.

Naye Mkuu wa Kitengo cha Ushirikiano na Maendeleo kwenye Ubalozi wa Sweden nchini, Maria Van Berlekom, akizungumza kwa Kiswalihili fasaha, amesema Wabunge hao, wa Sweden wamekuja kujionea hali halisi ya matumizi ya fedha za misaada ya kimaendeleo inayofadhiliwa na Sweden, ili kujiridhisha kama misaada yao inatumika vizuri na kwa malengo yaliyokusudiwa.

CRDB Microfinance ni kampuni tanzu ya Benki ya CRDB inayojishughulisha na huduma mbalimbali ikiwemo utoaji wa mikopo kwa wajasiliamali wadogo na wakati, huduma za bima, ushauri wa kiuchumi  nan die msambazaji mkuu wa huduma za Fahari Huduma hadi vijijini.

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger