Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumza na Wabunge kutoka
nchini Sweden (hawapo pichani) leo jijini Da es salaam wakati wa mkutano
uliofanyika Wizarani hapo, kuhusu ushirikiano wa kimaendeleo kati ya
Tanzania na Sweden. Kulia ni Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) Prof. Mussa Assad.
Waziri
wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akizungumzia vipaumbele vya
Serikali wakati wa mkutano na Wabunge kutoka nchini Sweden leo jijini
Dar es salaam kwa ziara ya kikazi nchini.
Waziri
wa Fedha na Mipango,Mhe. Dkt. Philip Mpango amekutana na Wabunge wa
Sweden katika ukumbi wa Wizara hiyo, kuzungumzia ushirikiano baina
Tanzania na Sweden.
Katika
mazungumzo yake na wabunge hao ambao wamewasili nchini kwa ziara ya
kikazi, Dkt. Mpango amesema Serikali ya Awamu ya Tano ipo makini na
inafanyakazi kwa ufanisi ili kuhakikisha Watanzania wanapata huduma
stahiki kutokana na rasilimali zilizopo nchini.
Amesema
Serikali imejipanga kuongeza kasi ya ukusanyaji mapato ya ndani ili
kuiwezesha nchi kujiendesha yenyewe na kuacha kutegemea misaada ya
wahisani.
Aidha,
amefafanua kuwa Tanzania imejipanga kuongeza vyanzo vya ukusanyaji
mapato pamoja na kuboresha vyanzo vilivyopo na kuhakikishakila
Mwananchi anayestahilikulipakodistahikianalipa kwa wakati.
“Ni
aibu kwa nchi yenye rasilimali za kutosha Wananchi wake kuishi katika
hali ya umasikini, tunachotakiwa ni kuboresha kilimo kwa sababu wananchi
wengi ndicho wanachotegemea”, alisema.
Akizungumzia
vipaumbele vya Serikali katika mkutano huo, Dkt. Mpango alisema mkazo
umewekwa zaidi katika kufanya mapinduzi ya viwanda, ambapo nchi
inaanzakuboresha viwanda vilivyopo hususani vile ambavyo hutumia
rasilimali zinazopatikana nchini kama zile zinazotokana na kilimo.
Aliongeza
kuwa katika kuboresha viwanda pia Serikali ipo katika hatua za
kuboresha soko la ndani na nje ya nchi kwa bidhaa zinazozalishwa na
viwanda hivyo.
Dkt.
Mpango alisema sambamba na kufanya mapinduzi ya viwanda, Tanzania
imejipanga kuboresha miundombinu ambapo mpaka sasa kuna miradi
mbalimbali ya maendeleo imeanzishwa kama mradi wa umeme vijijini.
Alisema
katika suala la umeme, nchi imeazimia kujikita katika uzalishaji wa
kutumia vyanzo vingine kama gesi asilia, jua na upepo kuliko kutegemea
maji pekee.
Kuhusu
sekta ya usafirishaji, Dkt. Mpango amesema Serikali imejipanga
kuboresha bandari zote nchini na kuzifanya ziwe za kisasa ili
kuhamasisha biashara za ndani na nje ya nchi kupitia bandari hizo.
Hata
hivyo, Dkt. Mpango alikiri kuwa uboreshaji wa reli ya kati ni
changamoto kwani reli hiyo haiwezi kuboreshwa kwa kutumia fedha za
bajeti ya Serikali pekee, hivyo Serikali inajitahidi kutafuta njia za
kufanikisha ujenzi huo.
Katika
mkutano huo, Dkt. Mpango alizungumzia suala la huduma za kijamii
alisema, nchi imejipanga kutoa elimu inayoendana na soko la ajira na
Serikali imeanza kutoa elimu ya msingi na sekondari bila malipo ili
kuwawezesha wananchi wengi kupata elimu.
Akizungumzia
suala la uchumi, Dkt. Mpango alisema hali ya uchumi kwa sasa ni nzuri
kwani pato la ndani la Taifa limefika asilimia 7 katika miaka ya hivi
karibuni.
Dkt.
Mpango alisema ili kufanikisha vipaumbele hivyo, ni lazima maadili na
nidhamu ya kazi vifuatwe na watendaji pamoja na watumishi wa umma katika
utekelezaji wa majukumu yao.
Aliongeza
kuwa Serikali ipo msatari wa mbele kupambana na rushwa na haitosita
kuhakikisha watu wote wanaohusika na rushwa wanachukuliwa hatua za
kisheria.
Kwa
upande Wabunge kutoka nchini Sweden, wakiongozwa na Mwenyekiti wa
Kamati ya Mambo ya Nje, Kenneth Forslund, wameipongeza Serikali ya Awamu
ya Tano kwa jitihada mbalimbali zinazochukuliwa katika ukusanyaji wa
mapato ya ndani na kutoa huduma za kijamii.
Tanzania
na Swede nzime kuwa na ushirikiano wa muda mrefu ambao umeifaidisha
Tanzania katika shughuli mbalimbali za maendeleo ikiwemo kuendeleza
miradi ya afya na umeme hususani vijijini, elimu pamoja na kusaidia
kukamilisha bajeti ya kila mwaka.
SHARE
No comments:
Post a Comment