RAIS mstaafu Jakaya Kikwete ameteuliwa na Dk. Nkosazana Dlamini Zuma, Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika kuwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika katika mchakato wa usuluhishi wa mgogoro wa Libya.
Kutokana na uteuzi huo uliotangazwa rasmi jana na AU jana katika kikao cha wakuu wa nchi za Afrika, Kikwete alikutana na Dk. Zuma makao makuu ya AU na kufanya naye mazungumzo kuhusu jukumu alilokabidhiwa.
Kikwete alimshukuru Dk. Zuma na wakuu wa nchi za AU kwa imani kubwa waliyoonesha kwake kwa kukabidhiwa jukumu hilo zito. Aliwashukuru pia wadau wa siasa nchini Libya kwa kuridhia uteuzi wake.
SHARE
No comments:
Post a Comment