Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akijitambulisha
kwa wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama kabla ya Kamati hiyo kuipokea taarifa ya Wizara hiyo katika
kikao cha kwanza cha Kamati hiyo baada ya kuundwa na Bunge hivi
karibuni. Wapili kushoto ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi
Mohamed Rajabu anayefuatia ni Makamu wake, Kanali Masoud Khamis. Kulia
kwa Masauni ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest
Rwegasira. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa
Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama, Balozi
Adadi Mohamed Rajabu akizungumza jambo na Wajumbe wa Kamati yake pamoja
na Watendaji Wakuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kikao
chao kwanza tangu Kamati hiyo iundwe na Bunge hivi karibuni. Wapili
kulia mstari wa mbele ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia
Hamad Masauni, na kulia kwake ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja
Jenerali Projest Rwegasira. Kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati hiyo,
Kanali Masoud Khamis. Kikao hicho kilifanyika katika Ukumbi wa Mikutano
wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni akitoa taarifa
ya Wizara katika kikao cha kwanza cha Kamati ya Kudumu ya Bunge ya
Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kikao hicho kilichohudhuriwa na Wajumbe
wa Kamati hiyo pamoja na Maafisa wa Wizara, kilifanyika katika Ukumbi
wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo. Kulia ni
Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu.
Baadhi
ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na
Usalama, pamoja na Wakuu wa Vyombo vya Ulinzi na Usalama na Maafisa wa
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, wakimsikiliza Naibu Waziri wa Wizara
hiyo, Injinia Hamad Masauni (hayupo pichani) alipokuwa anawasilisha
taarifa ya Wizara kwa Kamati hiyo katika kikao kilichofanyika katika
Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo.
Naibu
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Injinia Hamad Masauni (katikati) akiwa
na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Meja Jenerali Projest Rwegasira
wakiiweka sawa taarifa ya wizara yao kabla ya kuiwasilisha kwa wajumbe
wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama. Kulia
ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Balozi Adadi Mohamed Rajabu. Wajumbe wa
Kamati hiyo pamoja na Watendaji wa Wizara walikutana katika Ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Kisenga jijini Dar es Salaam leo, kwa ajili ya
kujadili masuala mbalimbali ya Ulinzi na Usalama. Picha zote na Wizara
ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
SHARE
No comments:
Post a Comment