Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo
(kushoto) akimkabidhi Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni, Bi. Grace
Mtesigwa (kulia) msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni
5 yaliyotolewa juzi kwa Shule ya Msingi Upendo iliyopo Manispaa ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB pia ilikabidhi madawati 53
kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar
es Salaam. Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakifurahia mara baada
ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye thamani ya shilingi
milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Shule ya Msingi Upendo wakiimba wimbo kwa
furaha mara baada ya shule yao kupokea msaada wa madawati 50 yenye
thamani ya shilingi milioni 5 kutoka Benki ya NMB jana jijini Dar es
Salaam. Meneja
wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo
(kulia) akizungumza wakati wa hafla ya Banki hiyo kukabidhi msaada wa
madawati 50 yenye thamani ya shilingi milioni 5 kwa Shule ya Msingi
Upendo iliyopo Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Benki ya NMB
pia ilikabidhi madawati mengine 53 kwa Shule ya Msingi Kibwegere iliyopo
Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam. Baadhi
ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Kibwegere wakiwa katika hafla ya
kukabidhiwa msaada wa madawati 53 yenye thamani ya shilingi milioni 5
kutoka Benki ya NMB juzi jijini Dar es Salaam. Katikati pichani ni
baadhi ya madawati hayo. Kutoka
kushoto ni Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Upendo, Yusuph Zanny,
Mwenyekiti wa Mtaa wa Mbezi Luis, Mwenyekiti Kamati ya Shule ya Shule ya
Msingi Upendo, Phillip Kimaro, Ofisa Elimu wa Manispaa ya Kinondoni,
Bi. Grace Mtesigwa, Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam na
Zanzibar, Bi. Vicky Bishubo wakiwa katika picha ya pamoja na wageni
waalikwa walioshiriki kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment