Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
(Kulia) akiteta jambo na Waziri wa Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na
Walemavu Mhe. Jenista Muhagama katika ufunguzi wa Mkutano wa nane wa
Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo wa siku
mbili umefunguliwa leo na unafanyika jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiongea na Vyombo mbalimbali vya Habari mara baada ya ufunguzi wa
Mkutano wa nane wa Mifuko ya Jamii Afrika Mashariki na Kati. Mkutano huo
wa siku mbili unafanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi
wa Masoko na Utafiti, Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa NHIF Rehani
Athumani akifuatilia mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Afrika Mashariki uliofanyika leo Jijini Dare s salaam.
Baadhi
ya washiriki waliohudhuria mkutano wa vyama vya mifuko ya Jamii Afrika
Mashariki na kati wakiwa wamesimama kumuaga mgeni rasmi Makamu wa Rais
Mhe.Samia Suluhu Hassan alipokuwa akifungua mkutano huo leo Jijini Dar
es Salaam.
Makamu
wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan akiwa katika picha ya pamoja na baadhi
ya mawaziri na manaibu waziri kutoka nchi mbalimbali za Afrika ya
Mashariki na Kati wakati wa mkutano wa Umoja wa Mifuko ya Hifadhi ya
Jamii Afrika Mashariki na kati leo Jijini Dar es Salaam.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akikabidhi cheti katika Mkutano wa Nane wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii
Afrika Mashariki na Kati. Makamu wa Rais amefungua rasmi mkutano huo leo
katika Ukumbi wa Benki Kuu.
………………………………………………………………………………………………………..
Na Jacquiline Mrisho MAELEZO
Makamu
wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan ameshauri kurasimishwa kwa ajira zisizo
rasmi ili ziweze kuchangia katika pato na maendeleo ya Taifa kwa kukuza
uchumi wa mtu mmoja na wa Taifa kiujumla.
Ametoa
ushauri huo Leo Jijini Dar es salaam wakati akifungua mkutano wa Umoja
wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii Afrika Mashariki na Kati amesema ili
kuwezesha kuzalisha ajira nyingi ni vyema kurasimisha ajira zisizo rasmi
ili kutoa nafasi nyingi kwa vijana kujiajiri na kuondokana na wimbi la
ukosefu wa ajira barani Afrika.
“Ili
wananchi waweze kujiamini na maisha yao ya baadae ni lazima wawe na
imani na ajira zao pamoja na hali nzuri ya kiuchumi,kukua kwa uchumi
ndio njia rahisi inayowezesha upatikanaji wa ajira.”
“Kuanzishwa
kwa Mifuko ya Jamii kumesaidia kuwainua wananchi kiuchumi,kijamii na
inawalinda watu wasipoteze ajira zao, na ndio sababu Mifuko hii
inajulikana kama “haki kwa watu wote” (Universal Right)” Alisema Mhe.
Samia.
Ameongeza
kuwa, ni lazima iundwe mikakati mizuri ya kukuza uchumi ambayo
itasaidia katika ukuzaji wa biashara,uwepo wa bajeti yenye
nguvu,kuwekeza katika miundo mbinu pamoja na kuwa na mifumo mizuri ya
kodi.
Aidha,amewaomba wanaohusika na utungaji wa sera za Mifuko ya Jamii kuzingatia sera zinazochochea ukuaji wa uchumi.
Mkutano
huu ulihudhuriwa na Mawaziri na Manaibu Waziri kutoka nchi mbalimbali
za Afrika Mashariki na Kati ,Naibu Gavana wa Benki kuu ya Tanzania,
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Duniani (ILO) ,wakurugenzi wa mabenki na
wawakilishi wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment