WADAU
mbalimbali,Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wanatarajia kukutana
kwenye Mkutano Mkuu wa 25 wa mwaka wa mfuko huo kwaajili ya kujadili
mambo mbalimbali yakiwemo ya uendelezaji wa sekta ya uhifadhi ya
jamii.Akizungumza na mtandao huu,jijini Dar es Salaam leo mchana wakati akitoa
taarifa hiyo, Meneja Uhusiano PPF, Lulu Mengele alisema kuwa mkutano
huo utafanyika Februari 11 na 12 mwaka huu katika ukumbi wa mikutano wa
Mwalimu Nyerere jijini hapa,huku ukihudhuriwa na wadau mbalimbali kutoka
ndani na nje ya mkoa wa Dar es Salaam.
Alisema
pamoja na kujadili uendelezaji huo pia watajadili mafanikio ya mfuko huo
kwa mwaka mzima na umuhimu wa kuzingatia mabadiliko, huku Kaulimbiu ya
mkutano huo ikiwa ni ‘Uendelezaji wa Sekta ya Hifadhi Jamii na Umuhimu
wa kuzingatia Mabadiliko’.
“Mkutano
huo utafanyika na wadau mbalimbali wakiwemo Wenyeviti na wajumbe wa
bodi, maofisa watendaji wakuu, wakurugenzi, wakuu wa vitengo, vyama vya
waajiri, ambapo baadhi ya Wanachama watapata fursa ya kutoa ushuhuda
kuhusu huduma za mfuko wa PPF” alisema Lulu
Wakati
huohuo, Mengele alizungumzia mfumo maalumu wa Wote Scheme ambao
unazihusisha sekta zisiyo rasmi na ule mfumo wa ziada uliopo kwenye
sekta iliyo rasmi.
Alifafanua
lengo kuu la mfumo huo kuwa ni kukidhi mahitaji na kutambua mchango na
ushiriki wa sekta isiyo rasmi kwenye uchumi na pia kutoa fursa
mbalimbali kwa wafanyakazi waliopo kwenye sekta rasmi ili kuwawezesha
kunufaika na mfumo huo kwa ajili ya kukuza shughuli mbalimbali za
kiuchumi na kijamii.
Kuhusu
nani anastahili kujiunga , Mengele alisema kila mtu au kikundi chenye
kipato na chenye mlengo wa kiuchumi kilichopo kwenye sekta isiyo rasmi
kama vile wakulima, wafugaji, wavuvi, mama lishe, waendesha bodaboda,
wajasiriamali, wadogo, wasanii, wanamichezo wachimbaji madini wadogo.
Ambapo
alisema kuwa jinsi ya kuchangia kiwango cha chini kwa mwezi ni sh.20,000
ambacho kinaweza kulipwa aidha moja kwa moja kwenye akaunti ya Mfuko wa
Pensheni wa PPF au kwa njia ya M-Pesa, Airtel money na Tigo pesa.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment