Mkurugenzi
wa Kampuni ya Msama Promotion Bw. Alex Msama akizungumza na waandishiwa
habari wakati alipotangaza viingilia vya tamasha la Pasaka
litakalofanyika katika mikoa ya Geita , Mwanza na Shinyanga, kushoto ni
Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha la Pasaka, Khamis Pembe.
………………………………………………………………………………………………………..
KAMPUNI
ya Msama Promotions imetangaza viingilio vya Tamasha la Pasaka mwaka
huu kuwa ni shilingi 5000 kwa wakubwa na shilingi 2000 kwa watoto.
Akizungumza
na Waandishi wa habari jana, Mwenyekiti wa Kamati ya maandalizi, Alex
Msama alisema viingilio hivyo vinaendana na tukio hilo ambalo mbali ya
kumuimbia na kumtukuza Mungu pia lina dhamira ya kusaidia jamii yenye
uhitaji maalum.
“Nawaomba wakazi wa mikoa Geita, Mwanza na Shinyanga kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha tamasha hilo,” alisema Msama.
Msama
alisema kupitia viingilio vya tamasha hilo wanatarajia kutoa kipaumbele
kwa wakazi wa mikoa itakayopitiwa na tamasha kwa baiskeli zaidi ya 100
za walemavu ambazo zitagawiwa mikoa mbalimbali.
Aidha Msama alisema waimbaji mbalimbali wamethibitisha kushiriki tamasha hilo ambao wanaendelea na mazoezi ya kujiweka sawa.
Naye
Mjumbe wa Kamati ya maandalizi ya tamasha hilo, Khamis Pembe alisema
wanaendelea na mikakati ya kuimarisha ulinzi kwa wakazi wa mikoa hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment