Na.Catherine Sungura-Nzega
Serikali
haitokuwa tayari kuwaona watumishi wa umma wachache wakinufaika na
kufaidi pesa za walipa kodi hususan wa kipatao cha chini na wale
maskinini
Hayo
yamesema wilayani hapa na Naibu Waziri wa Afya,Maendeleo ya
Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto, Dkt.Hamisi Kigwangwalla alipokuwa
akiwahutubia wananchi wa wilaya hiyo
Dkt.Kigwangwalla
alisema serikali ya awamu ya tano inawataka watumishi wote nchini
kufanya kazi za kuwahudumia wananchi na kuacha uzembe kwani awamu hii
haiwezi kuwavumilia watumishi wa namna hiyo.
“Serikali
haitowav umilia watumishi wazembe,hivyo tutaendelea kuwafungia mageti
na kuwashughulikia wale wazembe,tunataka watumishi wa umma wafanye kazi
ya kuwahudumia wananchi kwa ufanisi,mtumishi akizembea tutamtumbua
majipu,akichelewa tunamfungia geti na akiiba tunafilisi pamoja na
kumpeleka jela,hii ndiyo serikali ya hapa kazi tu”
Aidha
alisema serikali ya awamu ya tano inataka kero za wananchi zifanyiwe
kazi na kutekeleza ahadi zote za ilani ya uchaguzi ya ccm zinatimizwa.
“hatutomuonea
mtu,lakini tutafanyia kazi pale penye matatizo,tunataka Tanzania mpya
ya mwaka 2015 inakua,hatutaki hadithi wala ahadi”
Hatahivyo
aliwataka wazazi wote wenye watoto wenye umri wa kwenda shule
kuwapeleka watoto wao kuanza masomo kwani elimu kwa sasa ni bure na
hakuna michango yoyote.
“natoa
wito kwa walimu wote wasitoze michango yeyote wala ushuru kwa wazazi
wanaowapeleka kuwaandikisha watoto shule kwani shule zimepatiwa pesa za
kuendeshea shule hizo.
Dkt.
Kigwangwalla aliwakumbusha watumishi wa umma kujipanga na kama
watagundulika ni majipu bali hawatosita kuwatumbua hadi kina
kitoke,usaha na damu kutoka bila huruma.
SHARE
No comments:
Post a Comment