Mkuu wa Chuo kikuu cha Mzumbe Kampasi ya Dar es salaam Profesa Ganka Nyamsongoro akifungua Semina kwa ajili ya wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali semina iliyolenga programu ya UNIDO wakishirikiana na Chuo kikuu cha Mzumbe kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi kupata mafunzo ya ujuzi wa kazi.
Baadhi
ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na
wajasiliamali wakiwa katika semina hiyo iliyofanyika katika ukumbi wa
Peacock Hotel Dar
Mshauri wa UNIDO Bw. Mike Laizer akichangia jambo katika semina hiyo
Bw. Deosdadit Bernad Msimamizi wa Programu kutoka UNIDO akielezea kwa undani juu ya Programu hiyo
Baadhi ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali wakiendelea kufuatilia Semina
Profesa
Prosper Ngowi Msimamizi Mkuu wa Programu hiyo akieleza kwa kina nia na
malengo ya wao kufanya hivyo kwa kushirikiana na ‘SMEs’ ili kuwapa ujuzi
wa kazi wahitimu na wahitimu kutoa ujuzi wao waliokuwa nao ili kuweza
kukuwa zaidi
Wafanyabiashara,
wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na wajasiliamali
wakiwa wanaendelea kufuatilia semina hiyo kwa makini
Baadhi
ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na
wajasiliamali wakiwa wanauliza maswali na kuchangia mawazo katika
Semina hiyo
Mmoja
wa ‘Mentor’ katika programu hiyo Bw. Kaaya akiwa anatoa maelezo kwa
wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo vya uzalishaji na
wajasiliamali jinsi ambavyo watashirikiana katika kuwafundisha kazi
wahitimu hao pamoja na kushirikiana katika mambo mbalimbali
Picha
ya Pamoja kati ya wafanyabiashara, wamiliki wa viwanda vidogo vidogo
vya uzalishaji na wajasiliamali, Chuo kikuu cha Mzumbe na wawakilishi
kutoka UNIDO
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Profesa Ganka akifungua semina fupi na
wahitimu kutoka vyuo mbalimbali ambao ni watanzania katika programu
iliyo andaliwa na UNIDO ikiratibiwa na Chuo Kikuu cha Mzumbe juu ya
Mafunzo ya kazi ‘Internship’ ambayo yataanza hivi karibuni ambapo
wahitimu hao watatakiwa kufanya kazi kwa miezi minne katika viwanda
vidogo vidogo vya uzalishaji, wafanyabiashara na wajasiliamali
Msimamizi Mkuu wa Programu kutoka chuo kikuu cha Mzumbe Profesa Prosper Ngowi akiwaelezea wahitimu juu ya Programu hiyo
Baadhi
ya wahitimu wakiwa wanauliza maswali na kutaka ufafanuzi katika baadhi
ya maeneo ambayo walikuwa hawajayaelewa katika semina hiyo iliyofanyika
katika Chuo kikuu cha Mzumbe
Dkt.
Darleene Mutalemwa akitoa neno la Shukurani kwa wote wahitimu wote
waliofika katika semina hiyo kwa niaba ya UNIDO na Chuo kikuu cha Mzumbe
Wahitimu
wakiwa katika semina hiyo ya kupata maelekezo juu ya Programu ambayo
inalenga kuwapa Mafunzo ya kazi wahitimu iliyo andaliwa na UNIDO
ikiratibiwa na Chuo kikuu cha Mzumbe
SHARE
No comments:
Post a Comment