Mkurugenzi
wa chama cha waajiri Tanzania (ATE) Agrey Mlimka akiwa anafafanua
jambo katika mkutano wa siku moja wa kujadili changamoto mbalimbali
zinazo wakabili waajiri mkutano uliowashirikisha waajiri kutoka katika
sekta mbalimbali uliofanyika ndani ya hotel ya Kibo palace jijini Arusha
leo
wanachama
wa chama cha waajiri pamoja na wasio wanachama wa wakiwa wanajadili
kwa makini changamoto ambazo zinawakabili waajiri na jinsi ya kuzitatua .
Na Woinde Shizza,Arusha
Chama cha Waajiri nchini kimelalamikia vitendo vya rushwa
kuwa vikwazo katika biashara hivyo wameiomba serikali kukemea vitendo vya
rushwa pamoja na urasimu ili kuboresha mazingira mazuri ya biashara za kitaifa
na kimataifa.
Hayo yameelezwa na Mkurugenzi Mkuu wa Chama cha Waajiri (ATE),Aggrey Mlimuka akizungumza katika Mkutano Mkuu wa Waajiri
amesema kuwa serikali inapaswa kujenga mazingira bora kwa waajiri wanaotoa
nafasi za ajira ili kujenga uchumi
endelevu wa nchi
Mkurugenzi huyo
ameiomba serikali iondoe vikwazo kwa waajiri wanaoajiri wataalamu kutoka nje
kutokana na kukosekana kwa wataalamu hao nchini pamoja na kupunguza tozo kubwa
za mafunzo ya wafanyakazi ambayo ni asilimia
5%.
Kwa upande wake Afisa
Mwajiri wa Kampuni ya Utalii amesema kuwa kwa muda mrefu wamekua wakipata adha
kubwa wakati wa kuajiri watu kutoka nje ya nchi suala ambalo serikali inatambua
kuwa baadhi ya taaluma hazipatikani nchini hivyo kulazimika kuchukua wataalamu
kutoka nje.
SHARE
No comments:
Post a Comment