Na Bashir Yakub.
Ni muhimu
kujua tofauti ya kisheria ya
maneno ubatili na ubatilifu kabla ya
kujua lolote kuhusu hadhi/nafasi ya kisheria ya ndoa pasi na
tendo la ndoa. Ujuvi wa maneno ubatili na ubatilifu ndio
utakaopelekea kufahamika vyema kwa haya makala.
Kisheria kuna tofauti kati ya ubatili na ubatilifu.
1.TOFAUTI YA KISHERIA KATI YA UBATILI NA UBATILIFU.
( a ) UBATILI.
Maana ya ubatili kisheria ni kuwa jambo hilo haliruhusiwi kabisa.
Halitakiwi kutendwa kwa namna yoyote ile . Kwa lugha ya
kitaalam matendo haya huitwa “VOID ACTS”.
Ni matendo haramu kabisa.
Kwa mfano kwenye ndoa matendo haramu ni pamoja na mtu kutangaza ndoa na mtoto wake wa kuzaa, au mtu na mzazi wake,
au kutangaza ndoa ya jinsia moja au kutangaza ndoa na mtu mwenye umri mdogo. Kwa namna yoyote matendo haya ni batili(
void), haramu na hayaruhusiwi kwa namna yoyote.
( b ) UBATILIFU.
Maana
ya ubatilifu kisheria ni kuwa tendo linakuwa
si halali wala si haramu isipokuwa ili liwe halali au haramu litategemea uamuzi wa upande mmoja kati ya pande mbili zilizokubaliana.
Upande mmoja unaweza kuamua jambo liwe halali au liwe haramu
, nitatoa mfano.
Mtu akikuuzia gari ambalo liko tofauti na ulivyokuwa umemwagiza katika mkataba wenu tendo hilo sio halali wala sio
haramu/batili ila ni batilifu.
Hii ina maana kuwa ukiamua kulipokea gari hilo na kulikubali
hivyohivyo lilivyo basi umehalalisha tendo hilo na limekuwa halali.
Ukikataa kulipokea kwakuwa linapingana na kile kilicho kwenye makubaliano basi tendo hilo
la kuletewa gari lililo tofauti linakuwa haramu/batili.
Basi
ifahamike kuwa katika sheria yapo matendo ambayo si halali wala si haramu. Na haya kwa kitaalam huitwa”voidable acts”.
Na hicho ndicho kitakachoelezwa katika kujibu swali la nafasi ya
kisheria ya mtu ambaye hawezi kutekeleza tendo la ndoa.
2. KUTOWEZA KUTEKELEZA TENDO LA NDOA.
Sheria imesema kushindwa kutekeleza tendo la ndoa”incapable of consummating”.
Maana
ya hili ni kushindwa kabisa kutekeleza tendo la ndoa na sio uwezo mdogo katika kutekeleza tendo la ndoa.
Tofauti hii ni lazima ipambanuliwe bayana.
KUSOMA ZAIDI sheriayakub.blogspot.com
SHARE
No comments:
Post a Comment