TRA

TRA

Wednesday, March 23, 2016

BENKI YA BARLAYS YAMZAWADIA MSHINDI WA KAMPENI YA 'BARCLAYS PREMIER LEGUE'

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !

Wapili kutoka kulia ni Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa akizungumza na waandishi wa habarijijini Dar es Salaam leo na kuwapa zawadi zawadi wateja mbalimbali na mmoja kumpa hundi ya shilingi milioni sita na laki tisa kwa kujishindia safari ya kwenda uingereza kuungalia mpira wa ligi ya uingereza. Kulia ni Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather kutoka kushoto ni Mkuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma na Mshindi wa milioni sita na laki tisa kutoka Morogoro, Hamadi Chambo.
Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather akimkabidhi hundi ya shilingi milioni sita na laki tisa mshindi ambaye alitakiwa kwenda Uingereza kuangalia ligi ya uingereza lakini kwa sababu zilizo chini ya uwezo wa wadhamini hao kushindwa kumpeleka huko na kumkabidhi fedha hizo mshindi huyo, Hamadi Chambo kushoto. wengine ni  Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa na kuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma.
Washindi wengine wa zawadi kutoka benki ya Barclays wakiwa katika picha ya pamoja na kuu wa Matawi ya Barclays Tanzania, Emmanuel Katuma, Mkurugenzi wa wateja wa rejareja wa benki ya Bacclays, Kurmaran Pather na Mkuu wa kitengo cha bidhaa kwa wateja wa rejareja wa benki ya Barclays, Oscar Mwakyusa.Washindi hao wamechagua kuzawadiwa mipira ambayo ni Origino kutoka uingereza

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger