Na Mwandishi Wetu
MANISPAA ya Wilaya ya Temeke
jijini Dar es Salaam, imepokea mkopo wa sh bilioni 19.6 kwa ajili ya kuwalipa fidia
wakazi wa maeneo yatakayobomolewa ili kupisha mpango wa maendeleo na ustawi
jiji.
Mkopo huo utakaolipwa kwa
miaka sita una lengo la kufanikisha mradi mkubwa wa ujenzi na uboreshaji
miundombinu ya jiji uitwao Dar es Salaam Metropolitan Development Project
(DMDP).
Akizungumza na ujumbe wa
viongozi na madiwani wa wilaya ya Temeke ulioongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo,
Sophia Mjema, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei iliyotoa
mkopo huo alisema wanaunga mkono hatua za maendeleo zinazochukuliwa na Serikali
Kuu na Tamisemi.
Alisema fedha hizo zitatumika
kwenye ujenzi wa mtandao wa barabara za lami wenye urefu wa kilometa 81.63
ujenzi wa masoko ya kisasa, vituo vya mabasi ya kisasa, upimaji wa viwanja
2,000 eneo al Kijichi na kuweka huduma za msingi, ujenzi wa mifereji ya mvua
kilometa 22.4, dampo la kisasa eneo la Kisarawe na madaraja yanayounganisha
kata mbalimbali.
“Tumetoa mikopo ya maendeleo kama
huu kwenye halmashauri za Mwanza, Magu, Kinondoni, Mbeya na Mji wa Bukoba
ambapo jumla ya sh trilioni tatu ambazo ni karibu sawa na bajeti ya maendeleo
inayotengwa na serikali ambayo ni sh trilioni saba,” alisema Dk. Kimei.
Mjema aliwaonya watendaji
wanaohusika na mradi huo kutoongeza majina ya wanaotakiwa kulipwa huku
akisisitiza kwamba watakaobainika kuhujumu mradi huo na kutumia isivyostahili
mkopo huo, watafukuzwa kazi na kufikishwa mahakamani.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei akizungumza
katika hafla ya kutia saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa
ajili ya ulipaji fidia kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha
miundombinu katika Mamlaka za Serikali za Mitaa za jijini la Dar es
Salaam (DMDP). (Picha ha Francis Dande)
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB akizungumza katika hafla hiyo.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza katika hafla ya kutia
saini mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 kwa ajili ya ulipaji fidia
kwa wananchi wanaopisha mradi wa uboresha miundombinu katika Mamlaka za
Serikali za Mitaa za jijini la Dar es Salaam (DMDP).
Baadhi ya watumishi wa Manispaa ya Temeke.
Baadhi ya wafanyakazi wa Benki ya CRDB.
Baadhi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Baadhi ya Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika hafla hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kushoto), Naibu Mkurugenzi wa benki hiyo, Naibu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Bw. Saugata Bandyopadhya.
Meya
wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo (kulia), Mkurugenzi wa
Manispaa ya Temeke, Photidas Kagimbo (wa pili kulia), wakiwa katika
hafla hiyo.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (wa tatu kushto,
akikabidhi Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema mfano wa hundi yenye
thamani ya Shs. Bilioni 19.6 kwa ajili ya uboresha wa miundombinu katika
Mamlaka zaSerikali za Mitaa za Jijini la Dar es Salaam.
Mkurugenzi
Mtendaji wa Benki ya CRDB, Dk. Charles Kimei (kulia), akibadilishana
hati na Meya wa Manispaa ya Temeke, Abdallah Chaurembo baada ya kusaini
mkataba wa mkopo wa shs. bilioni 19.6 katika hafla iliyofanyika jijini
Dar es Salaam. Katikati anayeshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke,
Sophia Mjema.
SHARE
No comments:
Post a Comment