Mkuu
wa Magereza Mkoani Kagera, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Magereza,
Omar Mtiga(wa pili kushoto) akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza,
John Casmir Minja(wa tatu kulia) nyumba mbili za Askari wa Jeshi la
Magereza ambazo tayari zimekamilika katika eneo linakojengwa Gereza la
Wilaya ya Biharamulo(wa pili kulia) ni Mkuu wa Wilaya ya Chato, Mhe.
Shaaban Ntarambe.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja(suti nyeusi) akiwa na Wajumbe
wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Chato wakiaangalia moja ya
Bweni la kulala Wafungwa/Mahabusu ambalo tayari limekamilika katika eneo
linakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato Mkoani Geita. Kukamilika kwa
Gereza hilo kutasaidia kutatua tatizo la Msongamano wa Wafungwa na
Mahabusu katika Magereza ya Biharamulo na Gereza Muleba.
Mkuu
wa Gereza la Biharamulo, Mrakibu Mwandamizi wa Magereza, Gidion Kakulu
akimuonesha Kamishna Jenerali wa Magereza maeneo mbalimbali ya Gereza
hilo katika ziara yake ya Kikazi leo Machi 10, 2016. Wengine ni Maafisa
Waandamizi wa Jeshi hilo ambao wameambatana na Kamishna Jenerali wa
Magereza katika ziara yake ya kikazi.
Kamishna
Jenerali wa Magereza - CGP John Casmir Minja akisalimiana na Mkuu wa
Gereza Kuu Butimba, Mwanza Kamishna Msaidizi wa Magereza, Jaili
Mwamugunda alipowasili katika Uwanja wa Ndege wa Mwanza kabla ya kuanza
ziara yake ya kikazi Mkoani Kagera ambapo leo Machi 10, 2016 ametembelea
eneo kunakojengwa Gereza la Wilaya ya Chato lililopo Mkoani Geita
pamoja na Gereza la Wilaya ya Biharamulo(wengine) ni Maofisa wa Jeshi la
Magereza kutoka Ofisi ya Magereza Mkoani Mwanza.
Kamishna
Jenerali wa Magereza, John Casmir Minja akifurahia jambo pamoja na
Luteni Jenerali Mstaafu Samuel Ndomba walipokutana katika Kivuko cha
Busisi kabla ya kuendelea na safari kuekelea Mkoani Kagera(kulia) ni
Mkuu wa Magereza Mkoani Mwanza, Goleha Masunzu.
SHARE
No comments:
Post a Comment