Diamond
Platnumz amesema wasanii wengi wa Tanzania na Afrika Mashariki kiujumla
wanapotea kwenye ramani ya muziki kwasababu wanaendekeza mashauzi,
starehe na kutaka kujionesha.
Akizungumza kwenye kipindi cha Planet Bongo kinachorushwa na East Africa Radio, Diamond alisema:
“Unajua
wasanii wengi wanapoteza na kushuka kimuziki sababu ya starehe pamoja
na mashauzi. Unakuta mtu amepata mafanikio kidogo anaanza mashauzi na
kufanya starehe zisizo na tija, ndiyo maana mimi huwezi kuniona kwenye
starehe hata wasanii wa WCB ni hivyo hivyo.”
Katika hatua nyingine Diamond alimwelezea Shettah na kusema ni mfano mzuri.
“Mimi
namkubali sana Shettah kwani jamaa ni bahili sana anaweza kutoka
kufanya show na akakwambia sina pesa, hata gari yake aliyonunua juzi
amenunua kwa pesa zake sababu anakusanya pesa zake na kufanyia vitu vya
msingi. Sasa hivi Shettah anajenga nyumba yake na hiyo yote sababu si
mtu wa mashauzi na wala si mtu wa starehe.”
SHARE
No comments:
Post a Comment