Mkuu
wa Mkoa wa Pwani, Evarist Ndikilo akiongeza na wananchi wa kata ya Mkuza
na wafanyakazi wa Kampuni ya M-Power wakati wa ufunguzi wa ofisi ya
kampuni hiyo iliyopo kata ya Mkuza.(Picha na Peter Kimath)
KAMPUNI
ya M-Power inayotoa huduma ya usambazaji wa umeme wa jua nchini Tanzania na
Rwanda imesema itaendelea kutoa ajira kwa vijana wanaohitimu vyuo mbalimbali
ili kuweza kupambana na changamoto ya ajira hapa nchini
Akizungumza
na wananchi wa Kata ya Mkuza mkoa wa Pwani,katika hafla ya uzinduzi wa ofisi ya
M-Power,Meneja wa Usambazaji wa kampuni hiyo,Affred Kohi alisema kuwa licha ya
kutoa huduma ya umeme wa jua pia wanatoa ajira kwa vijana kutokana na idadi
wanayohitaji.
Kohi
alisema kuwa kampuni hiyo imeshatoa ajira kwa zaidi ya vijana 100,000 ambao ni
wahitimu katika vyuo mbambali hapa nchini,na kabla ya kuajriwa wanapitishwa
kwenye kituo chao cha mafunzo kilichopo
mjini Arusha.
Alisema kuwa wanatoa huduma kulingana na bajeti ya mteja kwani atakuwa analipia kiwango cha fedha kidogo sana kulingana na huduma aliyotaka mteja na malipo hayo hufanyika kwa njia ya simu bila makato yoyote na sio lazima mteja kufika ofisini kulipia.
Aliongeza kuwa kaya nyingi sehemu za vijijini hazina
kabisa nishati ya umeme ama upo ila sio wa kudumu kwa kipindi kirefu,na wengine
wanashindwa kumudu huduma ya umeme kutokana na gharama wanazotozwa kwenye vifaa
ama wanapohitaji kupata huduma hiyo.
Kwa upande wake Mrakibu wa Jeshi la Polisi,Bakar
Kawinga alipongeza huduma iliyotolewa na kampuni ya M-Power hapa nchini,hasa
kusaidia kuweka nishati ya umeme wa jua katika vituo vya polisi,vituo vya afya vilivyoko
pembezoni mwa mji na ambavyo havijafikiwa na tanesco
Kamanda Kawinga aliahidi jeshi la polisi mkoa wa
pwani kutoa ushirkiano na kampuni hiyo katika kulinda miundo mbinu ya kampuni
hiyo iliyowekwa sehemu mbalimbali ili kuhakikisha hakuna uharibifu wowote
utakaotokea.
SHARE
No comments:
Post a Comment