Na Avila Kakingo, Globu ya Jamii.
KAMPUNI ya HUSEA imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuazishwa kwake Machi mwaka huu kwa kutoa msaada wa vifaa vya hospitali na kuwapa zawadi akinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.
KAMPUNI ya HUSEA imeadhimisha mwaka mmoja tangu kuazishwa kwake Machi mwaka huu kwa kutoa msaada wa vifaa vya hospitali na kuwapa zawadi akinamama waliojifungua leo katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na wandishi wetu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA , Pamela
Maro amesema kuwa Kampuni hiyo inajishughulisha na Mipango miji, utoaji
ushauri bure kuhusiana na Ardhi, Upimaji wa Ardhi pamoja na uchoraji
ramani za nyumba, pia amesema kuwa ofisi za Kampuni ya kampuni
ya Husea zipo Sinza Palestina kwa yeyote anayetaka ushauri kuhusiana na
ardhi anaweza kufika maeneo hayo kujipatia ushauri bila malipo.
Pia
Pamela amewaasa wanawake waliotoka kujifungua leo na wanawake wote
wanaopenda kumiliki ardhi kisheria waende katika ofisi zao ili waweze
kupata ushauri wa bure kuhusiana na maswala ya ardhi.
Kwa upande wa Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza, Wandi Kariame amewapongeza wafanyakazi wa kampuni ya HUSEA kwa kuadhimisha mwaka mmoja leo.
Pia
amewashukuru kwa kuona mahitaji ya Hospitali hiyo na kuwapongeza
wanawake waliojifungua leo kwa kuwapa zawadi ikiwa ni kuadhimisha siku
iliyofunguliwa ofisi hiyo kwa kufikisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo
kwani wangeweza kwenda katika hospitali nyingine au kwenda kilabu cha
pombe (Bar) kwenda kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni yao kwa kunjwa na
kula vitu wanavyovitaka au kunywa pombe tuu lakini wamewaona wao.
Mratibu Huduma Tiba katika wodi ya wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza,
Faith Mdee akitoa maelekezo kwa wafanyakazi wa Kampuni ya Husea
inayojishughulisha na utoaji ushauri, upimaji wa viwanja, uchoraji
ramani za nyumba pamoja na mipango miji.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA,
Pamela Maro akimkabidhi Daktari Mkuu wa Hospitali ya Palestina Sinza,
Dkt. Wandi Kariame aadhi ya vifaa vinavyotumika katika uzalishaji
katika wodi la wazazi katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo.Kushoto ni Muuguzi katika wodi ya wazazi katika hospitali Palestina Sinza.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA, Pamela Maro pamoja na madaktari wa hospitali ya Palestina Sinza wakimkabidhi baadhi ya zawadi zilizotolewa na wafanyakazi wa kampuni ya Husea, mama aliyotoka kujifungua katika hospitali hiyo, Bahati Ramadhani.
Mfanyakazi wa Kampuni ya HUSEA akimwangalia mtoto aliyetoka kuzaliwa masaa machache yaliyopita.
Baadhi ya wazazi wakiwa wamewapakata watoto waliojifungua leo mara baada ya kupata zawadi na kampuni ya HUSEA jijini Dar es Salaam leo.
Mfanyakazi wa Kampuni ya HUSEA akimkabidhi
mama aliyetoka kujifungua mda mfupi kabla ya kupewa zawadi hiyo katika
hospitali ya Palestina Sinza leo jijini Dar es Salaa.
Mfanyakazi wa kampuni ya HUSEA akimkabidhi mama aliyejifungua kwa njia ya Operesheni katika hosipitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam.
Mama na mwana.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya HUSEA, Pamela Maro(Kushoto) akiwa na baaadhi ya wafanyakazi wa Kampuni ya HUSEA katika
picha ya pamoja mara baada ya kutoa zawadi kwa watoto walipozaliwa leo
katika hospitali ya Palestina Sinza jijini Dar es Salaam leo ikiwa ni
kuadhimisha mwaka mmoja wa kampuni hiyo tangu kuanzishwa.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
Picha na Avila Kakingo wa Globu ya Jamii.
SHARE
No comments:
Post a Comment