Mkurugenzi
wa Hospitali ya Walemavu CCBRT, Bi. Brenda Msangi akimueleza Spika wa
Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia) kuhusu
namna ya utendaji kazi hospitalini hapo. Spika alitembelea hospitali
hiyo kuangalia utendaji kazi kama mlezi wao.
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (mwenye tai nyekundu) akipokea machapisho
yanayohusu masuala ya walemavu kutoka kwa Afisa Mtetezi CCBRT wa masuala
ya walemavu, Bw. Fredrick Msigala wakati alipotembelea hospitali hiyo
kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai (wa pili kulia) akipata maelekezo juu ya namna
ya wagonjwa wa macho wanavyowekewa macho bandia (artificial eyes)
wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya kwanza akiwa ni Mlezi wa
Hospitali hiyo. Kulia ni ni Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Spika
wa Bunge la Jamhuri ya Muunganao wa Tanzania, Mhe. Job Ndugai (kulia)
akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya CCBRT Bw. Erwin
Telemans (kushoto) wakati alipotembelea hospitali hiyo kwa mara ya
kwanza akiwa ni Mlezi wa Hospitali hiyo.Katikati ni Katibu Mkuu Wizara
ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mpoki Ulisubisya.
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Wizara ya Afya nchini pamoja na Menejimenti ns Madaktari wa
CCBRT alipowatembelea kama mlezi wa Hospitali hiyo.
SHARE
No comments:
Post a Comment