Mkali
wa miondoko ya Mipasho, Khadija Kopa (kushoto), akiongea na kujigamba
jinsi alivyodhamiria kufanya makamuzi ya kufa mtu kwenye tamasha la
Amsha Mama Festival katika viwanja vya Mwembe-Yanga, Temeke jijini Dar
es Salaam kesho. Kulia ni Mratibu Mkuu wa tamsha hilo, Joe Kariuki,
akimsikiliza kwa makini msanii huyo kwenye kikao cha waandishi wa
habari kilichofanyika ndani ya Hoteli ya Travertine Magomeni jijini Dar
es Salaam.
Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo, Joe Kariuki, akisisitiza jambo juu ya tamasha hilo.
Mkali wa miondoko ya Singeli, Msaga Sumu, akielezea namna atakavyowapagawisha wakazi wa Temeke hiyo kesho.
Baadhi ya waandishi wa habari wakifuatilia kikao hicho katikahoteli ya Travertine.
………………………………………………………………………………………………….
MKONGWE
wa miondoko ya mipasho nchini, Khadija Kopa, na mkali wa Singeli, Msaga
Sumu, hatimaye wamejitokeza na kujigamba kuwa kesho wataonyesha maajabu
ya nguvu katika tamasha la Amsha Mama Festival litakalofanyika katika
Viwanja vya Mwembe-Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Wakizungumza
mbele ya waandishi wa habari ndani ya ukumbi wa Travertine, Magomeni
jijini Dar, Khadija Kopa na Msaga Sumu walisema kwamba kwa makamuzi
waliyojipanga nayo kesho kwenye tamasha hilo kuna hatari ya ‘kufia
jukwaani’ kwani wamejipanga kutoa burudani kwa wakazi wa Temeke kiasi
ambacho hawajawahi kukifanya kwenye maisha yao.
“Kusema
kweli sisi kwa pamoja tumejipanga kuwaburudisha mashabiki zetu wote
kwani tuna uhakika kama tutapewa muda mrefu wa kufanya shoo basi kuna
hatari ya kufia jukwaani kwani muziki wetu ni wa watu wa Temeke hivyo
hatuna budi kesho kufanya kila linalowezekana ili tu tuweke historia
mpya kupitia tamasha hili la Amsha Mama Festival”, alisema Kopa.
Kwa
upande wa Mratibu Mkuu wa Tamasha hilo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa
lebo ya Candy na Candy Records, Joe Kariuki, tamasha hilo
linalotarajiwa kufanyika mapema kesho ni mahususi kwa kuwaamsha wanawake
wote wa Afrika Mashariki na Kati ili waweze kupata nafasi ya kujituma
bila uoga katika biashara na kazi zao mbalimbali.
“Ukiachilia
mbali hilo la kuwaamsha kinamama pia kesho kutakuwa na wasanii kibao wa
hapa nchini wakitumbuiza, miongoni mwa wasanii hapo ni Juma Nature,
Khadija Kopa, Mr Blue, Snura, Msaga Sumu, Ali Chocky, Roma, Young Killer
na Tunda Man,” alisema Joe huku akiwataka watu wote wajitokeze kwa
wingi kwani tamasha hilo ni la bure.
SHARE
No comments:
Post a Comment