
Mabasi ya mwendo wa haraka kwenye jiji
la Dar es salaam yapo kwenye majaribio ya kuanza kazi hivi karibuni na
inawezekana ulijiuliza kama itakuwa ni chaguo lako upande Mabasi hayo au
daladala barabara ya pembeni, yaani kutakua na daladala zinazofanya
kazi kwenda na kutoka town japokuwa mabasi ya haraka yameanza kazi?
Taarifa ikufikie kwamba mabasi hayo
yatakapoanza daladala zote zitatoka na alielithibitisha hilo March 29
2016 ni meneja mawasiliano wa mamlaka ya udhibiti usafiri wa nchi kavu
na majini (SUMATRA) David Mziray wakati akijibu swali la mwandishi wa habari kuhusu kukosekana vituo kwenye barabara ya Morogoro.
>>>’huu
mradi wa mabasi yaendayo haraka utakapoanza mabasi ya daladala yote
yatatoka, ndio maana utaona mabasi mengi yanayotumia barabara hizi za
mchanganganyiko kwa maana magari ya kawaida na mabasi, hakuna vituo vya
daladala kwa kuwa hiki ni kipindi cha mpito, yakishaanza haya mabasi ya
mwendo wa haraka, huduma hizi za mabasi ya kawaida zitasimama’
David Mziray pia ameeleza taarifa ya
kukamatwa kwa magari zaidi ya 100 ndani ya siku nne kutokana na kuvunja
sheria ikiwemo kupandisha gharama za nauli za daladala na ukatishaji wa
safari >>> ‘Kati ya
hayo magari 105, 36 yameshafikishwa Mahakamani kwa ajili ya kusomewa
mashtaka na kuweza kujibu tuhuma wanazokabiliwa na wakibainika wana
makosa kutakuwa na faini, kupelekwa jela au vyote viwili’
SHARE
No comments:
Post a Comment