Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akizungumza na wananchi wa Ukonga
pamoja na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam kuhusu Mfuko wa Hiari
wa PSPF wakati wa Semina ya Ujasiriamali Ukonga jana jijini Dar es
Salaam
Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bw. Delphin Richard akifafanua jambo kwa wajasiriamali
kuhusu Mfuko wa Hiari wa PSPF jana jijini Dar es Salaam. Kushoto ni
Mkurugenzi wa Mjasiriamali kwanza Enterprises Dr. Didas Lunyungu
Wajasiriamali kutoka maeneo ya
Ukonga na maeneo mengine ya mji wa Dar es Salaam wakisikiliza kwa makini
elimu iliyokuwa ikitolewa kuhusu uchangiaji wa hiari katika Mfuko wa
Hiari wa PSPF wakati wa semina ya wajasiriamali jana jijini Dar es
Salaam
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu kwa wachangiaji wa hiari
katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa kuandikisha wachangiaji wapya
wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe akitoa elimu kwa wachangiaji wa hiari
katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakati wa kuandikisha wachangiaji wapya
wa mfuko huo jana jijini Dar es Salaam.
Afisa kutoka Mfuko wa Pensheni wa
PSPF Bw. Mrisho Ngongo (kulia) akitoa fomu za kujisajiri kwa
wachangiaji wapya wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF jana jijini Dar
es Salaam
Baadhi ya wanachama wa hiari
katika Mfuko wa Hiari wa PSPF wakiwa katika mstari kwa ajili ya
kukamilisha hatua za mwisho za kujisajiri katika mfuko huo jana jijini
Dar es Salaam
Afisa Masoko kutoka Mfuko wa
Pensheni wa PSPF Bibi. Sarah Adebe (kushoto) akikagua fomu za uanachama
wa hiari katika Mfuko wa Hiari wa PSPF baada ya kusajili wanachama wapya
jana jijini Dar es Salaam
Picha na: Genofeva Matemu – Maelezo
………………………………………………………………………………………………………………..
Na: Genofeva Matemu – Maelezo
Tarehe: 03/03/2016
Wananchi zaidi ya 500 kutoka zoni
ya ukonga jijini Dar es Salaam wamejitokeza na kujisajiri kuwa
wanachama wa hiari katika mfuko wa hiari wa PSPF ili kuweza kunufaika na
mafao yatolewayo na mfuko huo.
Wananchi hao walipata fursa ya
kujisajiri wakati wa semina ya ujasiriamali iliyofanyika siku ya jana
maeneo ya Ukonga jijini Dar es Salaam na kuudhuriwa na wananchi wapatao
1600 kutoka zoni ya Ukonga na maeneo mengine ya jiji la Dar es Salaam na
mikoa ya jirani.
Akizungumza wakati wa semina hiyo
Afisa Uendeshaji kutoka Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF)
Bw. Delphin Richard amesema kuwa mfuko wa hiari wa PSPF uliundwa kwa
ajili ya kutoa fursa kwa wananchi kuwa na akiba ya ziada kwa kutoa uhuru
kwa mwanachama kuchangia kwa kutegemea upatikanaji wa kipato cha ziada
kitakachomwezesha kujiwekea akiba.
Bw. Richard amesema kuwa lengo la
PSPF ni kushiriki katika masuala mbalimbali ya kijamii ili kuweza kutoa
elimu ya mfuko wa hiari wa PSPF hivyo kutoa nafasi kwa wajasiriamali,
wakulima, wafugaji, wafanyabiashara, na watu binafsi kuchangia katika
mfuko wa hiari kipato chao cha ziada kwa ajili ya akiba ya ziada.
Kwa upande wake Afisa Masoko
Bibi. Sarah Adebe amesema kuwa jamii imekua na muitikio mkubwa wa
kujisajiri katika mfuko wa hiari wa PSPF kwani mfuko huo unatoa huduma
kwa kuchangia gharama ndogo hivyo kuwanufaisha wanachama hasa wa kipato
cha chini.
Naye Mjasiriamali kutoka zoni ya
Ukonga Bi. Doris Kimaro amesema kuwa ujio wa elimu ya mfuko wa hiari wa
PSPF ni mafanikio makubwa katika familia yake kwani atatumia nafasi
aliyoipata kwa kuchangia kipato chake cha ziada ili aweze kunufaika na
fao la elimu litakalomuwezesha kukidhi mahitaji yake ya baadae.
Mfuko wa hiari wa PSPF umelenga
kusaidia jamii kwa kuwa na mafao saba ambayo ni fao la elimu, fao la
ujasiriamali, fao la uzeeni, fao la kifo, fao la ugonjwa/ulemavu, fao la
kujitoa na fao la matibabu.
SHARE
No comments:
Post a Comment