Waziri
wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Mwigulu Nchemba akizungumza na Makamu
Mkuu wa chuo za SUA (Sokoine University of Agriculture) alipofika
kwaajili ya kukutana na wataalam na uongozi wa SUA kwaajili ya kupokea
maoni yao kuelekea kilimo, ufugaji na uvuvi wa kisasa. "Transformation
of Agriculture".
Katika
kikao hicho,Wataalam kutoka SUA walisisitiza kuwa ili Tanzania iweze
kuondokana na kilimo holela,ni wakati muafaka sasa kama nchi kuamua
kuwekeza kwenye kilimo cha umwagiliaji na kuondoakana na kilimo cha
mvua,pia kuachana na jembe la mkono na wakati huo huo kuimarisha vituo
vya utafiti na kuzalisha mbegu kikanda.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia mfereji
ulioandaliwa kwaajili ya kusambaza maji kwenye shamba la utafiti wa
mbegu za Mpunga-Kilombero.Matumizi ya mifereji kwenye kilimo yanaondoa
mfumo wa kutegemea mvua ili mimea kupata maji na kukua kwa wakati. Mwigulu
Nchemba anatarajia kuendelea na ziara ya kukagua vituo vya Utafiti na
uzalishaji wa mbegu nchi nzima,lakini wakati huo huo atatembelea
mashamba ya mifugo na maeneo ya uvuvi wa samaki.
Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo na
mtafiti wa mbegu kutoka mmoja ya maafisa wa juu wa wakala mkuu wa aghala
la mbegu za ASA(Agricultural Seed Agency) Mkoani Morogoro.Waziri wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akikagua mbegu zilizopo kwenye ghala la ASA mkoani morogoro.Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akizungumza na watumishi
wa ASA(Agricultural Seeds Agency) wakati wa ziara hiyo,Kubwa
alilosisitiza ni uzalendo na kufanya kazi kwa kujituma.Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akipewa maelekezo kuhusu
malisho ya ng'ombe yanayopatikana kwenye kituo cha utafiti wa mifugo
-Morogoro(LITA).Waziri
wa Kilimo,Mifugo na Uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba akiangalia baadhi ya
ndama wa Ng"ombe waliopo kwenye shamba la Utafiti kwenye kituo cha
LITA-Morogoro.Picha/maelezo na festo Sanga Jr
SHARE
No comments:
Post a Comment