Kaimu
Afisa Mkuu wa wateja wadogo na kati NMB (kulia)- Bw. Abdulmajid Nsekela
akifurahia pamoja na Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja
Mkuu wa FastJet Bw. John Corse baada ya kukamilisha hafla ya
makubaliano hayo iliyofanyika katika hoteli ya Courtyard Protea jijini
Dar es Salaam.
Mtendaji
Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker na Meneja Mkuu wa Fastjet nchini Bw.
John Corse wakieka saini mkataba ambao utawanufaisha wateja wa NMB na
ambao sio wateja wa NMB kuweza kulipia tiketi za usafiri wa ndege
kupitia NMB Mobile na matawi ya benki yaliyopo nchi nzima.
Kaimu
Afisa Mkuu wa Kitengo cha Wateja wadogo na Kati wa NMB – Bw. Abdulmajid
Nsekela akifafanua jambo kwa waandishi wa habari jinsi gani wateja wa
NMB na ambao sio wateja wanaweza kununua tiketi kwa kupitia NMB mobile
na matawi ya NMB.
Sasa
wateja wa NMB na wasio wateja wa NMB wanaweza kufanya malipo ya tiketi
za kusafiria za Fastjet kupitia matawi ya NMB yaliyopo nchi nzima au kwa
kupitia NMB Mobile. Njia hizi za malipo zitawarahisishia wateja zaidi
ya milioni mbili wa benki ya NMB na zaidi ya wateja laki mbili wa
kampuni ya ndege ya Fastjet kununua tiketi zao za kusafiria kwa urahisi
zaidi. Kwa wale wateja wa NMB, wanaweza kukamilisha manunuzi ya tiketi
kwa kutumia NMB mobile au kupitia zaidi ya matawi 170 ya NMB yaliyopo
nchi nzima.
Akiongea
na waandishi wa habari, Mtendaji Mkuu wa NMB Bi. Ineke Bussemaker
alisema,”Tunayo furaha kushirikiana na fastjet ambayo ni kampuni kubwa
ya ndege na yenye gharama nafuu nchini hivyo tunaamini kwamba
ushirikiano huu utasaidia kuleta huduma zetu karibu zaidi na watu
kupitia mtandao na matawi yetu nchini”.
Kulipia
tiketi ni rahisi sana, unachotakiwa kufanya ni kufanya maandalizi y
safari kupitia tovuti ya fastjet au vituo vyao vya mauzo ambapo utapata
namba ya kumbukumbu yenye tarakimu nane. Ukishapata hii namba ya
kumbukumbu, kwa wateja wa NMB unaweza kulipia kwa kupitia NMB mobile
Piga *150*66# kisha chagua Malipo ya Bili halafu chagua Fastjet.
Kwa
wateja wasio wa NMB, wanaweza kutembelea tawi lolote la NMB ili kufanya
malipo. Ukishafanya malipo, utapata SMS ya uthibitisho wa malipo pamoja
na ticket itakayotumwa kwenye barua pepe ambayo utakua umeisajili wakati
wa kupanga safari. Hakikisha una namba yako ya kumbukumbu wakati wote
ili ikuwezeshe kufanya malipo popote ulipo.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment