Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako
akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu
waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halmashauri kumi
zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesisitiza fedha za Elimu ambazo
zimetolewa na Serikali kama zawadi katika Halmashauri mbalimbali zilizofanya vizuri
katika Sekta ya Elimu zitumike vizuri.
Profesa Ndalichako ameyasema hayo leo wakati wa kutoa zawadi kwa Halmashauri
10 ambazo zimepokea Shilingi Bilioni 15.5.
Halmashauri hizo ni Mbinga, Chato, Busega, Lushoto, Niyankasi,
Liwale, Sikonge, Mbarali, Mpanda, pamoja naTabora.
Pia, Profesa Ndalichako amezitaja Halmashauri 10 za mwisho kuwa
ni Rombo, Kiteto, Meatu, Mafinga, Kasulu, Butihama, Wanging’ombe, Mbozi na Makambako.
Kwa upande wake, WaziriwaNchi, Ofisi ya Rais anayeshughulikia
Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mhe.George Simbachawene amezitaka Halmashauri
hizo ambazo zimefanya vizuri na kupata zawadi hiyo ya fedha kuzitumia vizuri fedha
hizo na kuhakikisha Elimu Bora inapatikana.
Waziri
wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce
Ndalichako(kulia) akimkabidhi hundi bilioni 15,532,905.10 Waziri wa nchi
ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George Simbachawane
wakati wa hafla ya kukabidhi zawadi kwa halmashauri kumi zilizofanya
vizuri kielimu katika ukumbi wa Makumbusho ya Taifa jijini Dar es Salaam
leo.
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya
akionesha cheti alichopewa kama halmashauri iliyoshika nafasi ya kwanza
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Mbarali Bw. Yeremiah Tito Mahinya akipokea cheti
pamoja na zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya halmashauri ya wilaya ya
Mbarali kufanya vizuri katika suala la elimu. Wa pili kutoka kulia ni
Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George
Simbachawane
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Bw, Ahmada .A. Suleman
akipokea zawadi kutoka kwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na
Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako baada ya wilaya hiyo kufanya vizuri
kielimu, wa pili kutoka kulia ni Waziri wa nchi ofisi ya Rais Tawala za
mikoa na serikali za mtaa, George Simbachawane
Waziri
wa nchi ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mtaa,George
Simbachawane akizungumza na wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na
maafisa elimu waliofika kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa
halimashauri kumi zilizofanya vizuri kielimu leo katika ukumbi wa
Makumbusho jijini Dar
Kaimu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbinga Jobu Andindilile Mwalukosya akitoa
neno la shkukrani kwa niaba ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja
na maafisa elimu waliofika kwenye hafla fupi ya utoaji zawadi kwa
halmashauri zilizofanya vizuri.
Baadhi
ya wakurugenzi, makaimu wakurugenzi pamoja na maafisa elimu waliofika
kwenye hafla ya utoaji wa zawadi kwa halimashauri kumi zilizofanya
vizuri kielimu leo katika ukumbi wa Makumbusho jijini Dar
Picha ya Pamoja.
Kaimu
Afisa elimu MsingiMoses Ndanzlama(kushoto), Afisa Elimu Sekondari Bi.
Claudia Kita(katikati) pamoja na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mbarali
Bw. Yeremiah Tito Mahinya wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kupewa
zawadi ya Cheti.
SHARE
No comments:
Post a Comment