WABUNGE wa Viti Maalum watatu
wameingia baada ya uchaguzi majimbo yote kukamilika ambapo Chama cha
Mapinduzi (CCM) kimepata viti maalum viwili na Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (Chadema) mmoja.
Akizungumza leo na waandishi wa
habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi
(NEC), Jaji Mstaafu ,Damian Lubuva amesema kuwa uchaguzi umekamilika
katika majimbo nane kwa kuwa na majimbo ya Tanzania Bara saba na
Zanzibar Moja ambalo ni Jimbo la Kitope Upele.
Viti vya wabunge wa viti maalum wanatokana na kura za jumla za wabunge wote na kuweza kupatikana viti hivyo.
Waliopatikana katika mchanganuo wa viti maalum ni, Ritha Kabati (CCM), Oliver Semunguruka (CCM) pamoja na Lucy Owenya (Chadema).
Lubuva amesema kuwa kufikia hapo
ndipo uchaguzi umekamilika kutokana na viti hiyo kupatikana na kufanya
kuwa viti maalumu 113 katika mgawanyo wa viti hivyo ni Chama cha
Mapinduzi (CCM) Viti 66, cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) viti
35 pamoja na Chama cha Wananchi (CUF) viti 10.
Amesema kuwa kutokana na chaguzi zinazoendelea NEC ndiwe iwe sehemu ya usimamizi wa chaguzi zote.
Idadi kura za wabunge CCM katika uchaguzi ambazo zilibaki kutokana wagombea kufariki na kuarishwa kumeongeza viti maalum viwili.
SHARE
No comments:
Post a Comment