Serikali
kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo imezishauri
Taasisi za Kibenki zilizopo nchini kuanzisha timu na vilabu vya michezo
ili kukuza michezo pamoja na kuongeza fursa za ajira kwa vijana walio
wengi ambao wana vipaji lakini hawana timu za kuwaendeleza.
Hayo
yamebainishwa kupitia kwa Waziri mwenye dhamana, Mh. Nape Nnauye
mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam wakati wa kukabidhi zawadi
mbalimbali ikiwemo tuzo za wachezaji bora walioshinda katika michezo
maalum ya BRAZUKA KIBENKI iliyoandaliwa na benki ya Barclays na wadau
wengine.
Waziri
Nape amebainisha kuwa, Nia ya Serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha
inakuza michezo na kuwa na fursa za kiuchumi kupitia michezo hivyo
taasisi hizo zinazo fursa ya kuongeza ajira na ustawi mzuri wa michezo
endapo zitaanzisha timu za michezo na kimashindano kwani zinaweza na
zinao wajibu huo.
Kwa
mujibu wa Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya alieleza kuwa,
jumla ya timu 16 zilishiriki huku ikianza 28 Novemba 2015 na kufikia
tamati 20 Februari 2016 ilikuwa ni ya aina yake na kutoa mwangaza wa
kimaendeleo wa kimichezo ambapo pia imesaidia kuimarisha afya,
ushikamano na undugu kwa baina ya wachezaji na washangiliaji ambao wengi
wao walitoka katika mabenki shiriki 15 ikiwemo matawi yao ya Tanzania
Bara na Visiwani.
Katika
tukio hilo, washindi mbalimbali walipatiwa vyeti vya shukrani hii ni
pamoja na wadhamini wa mashindano hayo ikiwemo kutoka mabenki, kampuni
ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) na makampuni
mengine walipewa vyeti vya shukrani katika kufanikisha michuano hiyo.
Imeandaliwa na Andrew Chale,Modewjiblog/MO tv)
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Bw.Zainul Mzige (kulia) akikabidhi cheti cha ushindi kwa Mchezaji Nuhu Mkuchu kutoka benki ya NMB.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo ya golikipa bora, Gabriel Bernard.
Waziri
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Nape Nnauye akikabidhi tuzo
ya mfungaji bora mchezaji kutoka benki ya NMB, Ahmed Nassoro.
Baadhi ya washiriki na wageni mbalimbali walifika katika tukio hilo...
Mratibu wa michuano hiyo Brazuka Kibenki, Bi. Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi wa michuano hiyo..
Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mshindi..
Waratibu
wa mashindano ya Brazuka Kibenki, Bi.Nasikiwa Berya akiwa na Raymond
Bunyinyiga wakifurahia jambo kutoka kwa Waziri wa Habari, Nape Nnauye.
(Hayupo pichani).
Waziri Nape akimkabidhi tuzo ya mchezaji Bora, Ahmed Nassoro.
Rais
wa shirikisho la Soka nchini, (TFF), Jamal Malinzi akikabidhi cheti cha
ushind kwa moja ya washiriki wa michuano ya Brazuka Kibenki.
Mratibu wa michuano hiyo, Nasikiwa Berya akikabidhi cheti kwa mshiriki..
Baadhi ya washiriki..
zoezi likiendelea..
Utoaji wa vyeti ukiendelea..
Waziri
Nape akimkabidho tuzo, Kocha Bora, Bw. Mohamed Hussen 'Machinga' ambaye
aliwahi kuwa mchezaji wa timu za Taifa na klabu kubwa za Tanzania
ikiwemo Simba.
Mwakilishi
kutoka MeTL Group, Zainul Mzige akikabidhi cheti kwa mmoja wa washindi
wa michuano ya Brazuka Kibenki. Zainul alikabidhi cheti hicho
akimwakilisha Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya Mohammed
Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group), Mohammed Dewji 'MO'.
Waziri
Nape akimkabidhi cheti Rais wa TFF, Jamali Malinzi, ambapo cheti hicho
ni maalum kwa TFF kuongeza mchango wao kaatika kukuza michezo nchini..
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Rais wa TFF akikabidhi tuzo hizo
Utoaji wa tuzo hizo ukiendelea..
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
wageni waalikwa na washiriki kutoka mabenki mbalimbali..
Waziri Nape akitoa tuzo hizo..
Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige akitoa vyeti kwa washiriki
Baadhi ya washindi walifanikiwa kutwaa tuzo hizo za Brazuka Kibenki kutoka benki ya NMB.
Wachezaji bora 11, wakipata picha ya pamoja..
Waziri Nape Nnauye akitoa nasaha fupi katika tukio hilo..
Mwandishi
Mwandamizi wa habari wa mtandao wa Modewjiblog, Bw. Andrew Chale akiwa
katika picha ya pamoja na Mwakilishi kutoka MeTL Group, Zainul Mzige.
Baadhi wa washriki na washindi wa Brazuka Kibenki..
Hapa ilikuwa ni furaha kwa washiriki katika tukio hilo la Brazuka Kibenki..
Ilikuwa ni mwendo wa kucheza na kufurahia Kibrazuka..
Waziri
Nape akipeana mkono naMwakilishi wa MeTL Group, Zainul Mzige katika
meza kuu ya wageni waalikwa. Zainul Mzige alimwakilisha Mkurugenzi
Mtendaji Mkuu wa MeTL Group, Mohammed Dewji 'MO'.
Baadhi ya washiriki wakipata picha za ukumbusho katika tukio hilo.
SHARE
No comments:
Post a Comment