Afisa
Mtendaji Mkuu wa Benjamin Mkapa Foundation, Dk. Ellen Mkondya Senkoro
akiongea na waandishi wa habari kutangaza maadhimisho ya miaka kumi ya
taasisi hiyo pamoja na shughuli mbalimbali zitazoambatana na maadhimisho
hayo jijini Dar es salaam jana. Taasisi hiyo imekuwa kinara katika
kuongoza jitihada za kuimarisha utoaji huduma za afya nchini katika
miaka kumi iliyopita. Kulia kwake ni Mkurugenzi wa Programu za Taasisi
hiyo Raheli Sheiza.
Taasisi
ya Benjamin Mkapa (BMF) imeendelea kutekeleza kutekeleza jitihada za
serikali ya Tanzania na washirika wake katika kuimarisha utoaji huduma
za afya katika maeneo yasiyopata huduma ya uhakika na mwezi Aprili 2016,
itaadhimisha miaka kumi tangu kuanzishwa Aprili 2006 na Rais Mstaafu wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzaniania, Mhe. Benjamin William Mkapa.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa BMF, Dk. Ellen Mkondya-Senkoro amesema kwenye mkutano
na waandishi wa habari leo , kauli mbiu ya maadhimisho hayo ya miaka
kumi ni “Miaka 10 – Tumejituma, Tumeaminika na Tumeweza”.
Taasisi
ina furahia kuweza kubadilisha maisha na afya za mamilioni ya
Watanzania ambao wamefikiwa moja kwa moja na ambao hawakufikiwa moja kwa
moja ya Taasisi.
Ameongeza
kwamba “Ikiwa ni sehemu ya maadhimisho hayo, Taasisi ya Benjamin Mkapa
itafanya shughuli mbalimbali za kijamii kuanzia March 2016 hadi mwisho
wa Aprili 2016.
Shughuli
hizo ni pamoja na utoaji huduma za afya kwa jamii, kutembelea maeneo
mbalimbali ambayo yamekuwa yakihudumiwa na taasisi, mkutano wa wadau, na
chakula cha usiku kuchangisha fedha.
Katika
kipidi hiki tutawatambua na kuwapa tuzo watu mbalimbali na taasisi
ambazo zimechangia ukuaji na mafanikio ya taasisi. Dk. Ellen alisema
“Bodi ya Wadhamini ya BMF, Wafanyakazi pamoja na familia zao watachangia
damu kwenye.
Hospitali
ya Taifa ya Muhimbili ikiwa nia mojawapo kuwasaidia watoto wenye
maradhi, akina mama wajawazito na wagonjwa wanaohitaji damu ili kuweza
kupona.
Pia
tutatoa elimu, ushauri nasaha na kuwapima VVU wagonjwa ambao wao kwenye
vituo vya afya vya umma kwenye mikoa ya Rukwa na Simiyu. Elimu ya afya
kuhusiana na Ukimwi na afya ya uzazi pia vitatolewa kwenye shule mbili
kaika mikoa hiyo”.
Katika
miaka kumi, taasisi ina fahari kuweza kubuni mbinu endelevu za kutatua
changamoto za kitaifa kwenye sekta ya afya “Tunaona fahari kuweza kutoa
ajira kwa zaidi ya watoa huduma za afya 1,100 ambao wamehudumia maeneo
yenye uhitaji mkubwa, kutoa nafasi za masomo kwa wanafunzi 1,000
wanaosoma kozi za elimu ya afya na kuweza kuwapa motisha watumishi wa
sekta ya afya kwa kuwajengea nyumba 480 za kuishi katika vituo vya afya
vijijini. Taasisi pia imeweza kuwafikia watumishi wa huduma ya afya
zaidi ya 800 na kuwapa mafunzo kuhusu utoaji huduma bora za afya kuhusu
ukimwi na afya ya uzazi”, alisema Dk. Mkondya-Senkoro.
Uchangishaji
fedha tayari unaendelea ambapo makampuni mbalimbali yameonyesha nia,
mengine yametoa ahadi na kutoa fedha pamoja na mali na makampuni hayo ni
pamoja na Mohammed Enterprises Tanzania Ltd, Bank M, Clouds Media Group
na wengine. Tunatarajia kupata ahadi zaidi kupitia hafla maalum ya
chakula cha jioni shughuli ambayo itahudhuriwa na wageni waalikwa 150.
Katika
hafla hiyo Taasisi ya Benjamin Mkapa imelenga kuchangisha shilingi
bilioni moja ikiwa ni sehemu ya bajeti yake ya mwaka wa Fedha hizo
zitawanufaisha Watanzania kupitia uimarishwaji wa nguvu kazi katika
sekta ya afya na huduma nyingine za afya hususani kwenye ukimwi, uzazi,
na afya mama na mtoto. Vile vile, taasisi itaitumia hafla hiyo kuzindua
jina lake jipya litakalojulikana kama “ “Benjamin W. Mkapa Foundation”
na kuondokana na “ Benjamin W. Mkapa HIV/AIDS Foundation”. Dr.
Mkondya-Senkoro aliongeza: “Katika jitihada zetu kuwa endelevu, kuongeza
ukuaji, ili kuendana na mazingira yanayobadilika kitaifa na kimataifa
ikiwemo maendeleo ya sekta ya afya, kuanzia tarehe 2 Novemba 2015,
tumebadilisha jina letu kuwa “The Benjamin William Mkapa Foundation
(BMF)”.
Mabadiliko
haya ni kutokana na lengo la taasisi kupanua wigo na kutekeleza
programu katika maeneo mengi zaidi ya ukimwi. Malengo makuu ya taasisi
hii yatabakia vilevile ikiwa ni kuwaletea matumaini Watanzania waishio
mazingira duni”.
SHARE
No comments:
Post a Comment