TRA

TRA

Friday, March 4, 2016

TAARIFA FUPI KUHUSU ZIARA YA RAIS WA VIETNAM NCHINI TANZANIA 9-10 MACHI 2016

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


logo
Utangulizi
Rais wa Jamhuri ya Kisoshalisti ya Vietnam Mheshimiwa Truong Tan Sang anatarajiwa kufanya ziara rasmi nchini tarehe 9 Machi 2016.  Madhumuni ya  ziara hiyo ni kukuza uhusiano baina ya Vietnam na Tanzania mbao umedumu kwa zaidi ya miaka hamsini tangu kuanzishwa kwake pamoja ‎Kufungua maeneo mapya ya Ushirikiano wa kiuchumi baina ya Tanzania na Vietnam. Hii ni ziara ya kwanza ya kiongozi huyo Barani Afrika tangu aingie madarakani mwaka 2011, ambapo nchi nyingine anayotarajiwa kutembelea ni Mozambique. Rais Truong anatarajiwa kufuatana na mke wake Bi Mai Thi Hahn, mawaziri 4 wanaoshughulika na sekta za  Kilimo, Mawasiliano Uwekezaji, Afya Viwanda na Biashara.  Aidha mgeni huyo atafuatana na ujumbe wa wafanyabiashara 30 kutoka Vietnam.  
Shughuli za msingi zitakazofanyika kwenye ziara
  • Wakati wa ziara hiyo Rais Truong Tang San atafanya mazungumzo rasmi na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. John Pombe Joseph Magufuli Ikulu jijini Dar-es-Salaam.
  • Aidha, Rais Truong pia atapata fursa ya kutembelea eneo la EPZ la Ubungo kuangalia viwanda mbalimbali vinavyozalisha bidhaa za kuuza nje ya
  • Baada ya kutembelea EPZA Rais Truong atahudhuria mkutano wa biashara na uwekezaji katika ukumbi wa mikutano wa Julius Nyerere. Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na taasisi za umma na sekta binafsi kutoka Tanzania na Vietnam.
  • Rais Truong atamaliza ratiba yake kwa kuhudhuria dhifa ya Taifa itakayoandaliwa kwa heshima yake na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk.John Pombe Joseph Magufuli.
Wasifu wa Rais wa Vietnam‎
  • M‎heshimiwa Truong Tan Sang amezaliwa tarehe 21 January 1949 katika Jimbo la Long An nchini Vietnam. Amepata Elimu ya Juu kutoka taasisi ya national Academy of Public Administration ya Vietnam ambako alipata Shahada ya kwanza ya Sanaa na Sheria.
  • Kutokea mwaka 1966 hadi 1996 Mheshimiwa Truong ameshika nafasi mbalimbali za utendaji  katika Chama Tawala cha kikomunisti cha Vietnam.
  • Mwaka 1996 Mhe Truong alichaguliwa kuwa Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Tawala na Katibu wa Chama hicho katika Jimbo la Ho Chi minh hadi mwaka 2000 ambapo aliachia wadhifa wa katibu Mkuu wa Jimbo na kuendelea na nafasi ya ujumbe wa Kamati kuu ya Chama tawala hadi tarehe 25 Julai 2011 apochaguliwa na Bunge la Vietnam kuwa Rais wa Vietnam.
  • Mhe Truong amemuoa Bi mai Thi Hanh  na wamejaaliwa mtoto mmoja.
Taarifa Muhimu Kuhusu Vietnam‎

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger