
Waziri wa
Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akizindua rasmi
albam mpya ya mwimbaji Goodluck wakati wa tamasha la Pasaka
lililofanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza leo na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa mkoa wa Mwanza , Wabunge pamoja na
Maaskofu wa makanisa ya Mwanza.
Tamasha
hilo ambalo limehudhuriwa na mashabiki wengi mkoani humo limetumbuizwa
na waimbaji mbalimbali wa nyimbo za injili kutoka hapa nchini na nchi
jirani za Zambia na Kenya, waimbaji hao ni Upendo Nkone , Martha baraka ,
Jesca BM, Joshua Mlelwa , Tumsifu Rufutu, Christopher Mwahangila,
Jeniffer Mgendi, Bonny Mwaiteje, Goodluck ambaye amezindua albam yake
mpya na waimbaji Faustine Munishi kutoka nchini Kenya, Solomon Mukubwa
kutoka Nchini Kenya pamoja na Ephraim Sekereti kutoka nchini Zambia wote
kwa pamoja wamefanya maonesha mazuri yaliyopagawisha mashabiki wa
muziki wa injili katika uwanja wa CCM Kirumba na kuwafanya wacheze kila
wakati, katika picha kulia ni mwimbaji Goodluck na kushoto ni Bw. Alex
Msama Mkurugenzi wa kampuni ya Msama Promotion inayoandaa matamasha
hayo.
Tamasha
hilo litaendelea kesho kwa onesho kabambe linalotarajiwa kufanyika
mjini Kahama mkoani Shinyanga baada ya kumaliza maonyesho mawili
katika mikoa ya Geita na Mwanza.(PICHA NA JOHN
BUKUKU-FULLSHANGWE-MWANZA)

Waziri wa
Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye wa nne kutoka kulia
akimsikiliza Mkuu wa mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela alipokuwa
akimkaribisha rasmi ili kutoa salam zake kutoka kwa serikali.

Waziri wa
Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishiriki katika
sala maalum ya kuombea albam ya mwimbaji Goodluck wa pili kutoka kulia
iliyotolewa na maaskofu wa mwanza kabla ya kuizindua

Waziri wa
Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe.Nape Nnauye akishuka kutoka
jukwaani kwa ajili ya kuizindua rasmi albam hiyo na kutoa salaam za
serikali katika tamasha la Pasaka.

Mkuu wa
mkoa wa Mwanza Mh. John Mongela akipokewa na Mkuu wa wilaya ya Nyamagana
Mh. Baraka Konisaga kushoto na Mkurugenzi wa Msama Promotion Bw. Alex
Msama wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

Mkuu wa
wilaya ya Nyamagana Mh. Baraka Konisaga akipokewa na Mkurugenzi wa
Msama Promotion Bw. Alex Msama wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM
Kirumba jijini Mwanza.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment