Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akizungumza jana katika Mkutano wa nane wa wadau wa LAPF unaoendelea jijini Arusha katika ukumbi wa AICC ambapo alikuwa mgeni rasmi mbali na mambo mengine,aliitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kutoa mafao kwa wakati pindi wanachama wake wanapostaafu ili kuhakikisha kuwa wastaafu wanapata mafao yao, kwani wengi wao wanakabiliwa na msongo wa mawazo kutokana na ugumu wa maisha unaowakabili baada ya kustaafu wanashindwa kujimudu kutokana na kukosa mafao yao(Habari Picha na Pamela Mollel wa jamiiblog Arusha)
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama ameitaka mifuko ya hifadhi ya jamii kuwekeza kwenye viwanda ili kuunga mkono msimamo wa serikali kuanzisha uchumi wa viwanda utakaotengeneza ajira na kuchochea maendeleo ya nchi
Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa Mifuko ya hifadhi ya jamii imekua chachu ya maendeleo ya taifa kutokana na uwekezaji unaofanywa na mifuko hiyo pamoja na mikopo mbalimbali inayotolewa kwa wanachama kujikwamua kimaisha
Mkuu wa mkoa wa Arusha Daudi Felix Ntibenda akizungumza katika mkutano huo jijini Arusha
Afisa Masoko wa LPF James Mlowe akizungumza katika mkutano huo ambapo alisema kuwa tayari mfuko huo umeanzisha mkopo wa maisha popote na LAPF ambao unalenga kuwasaidia watumishi wa umma hususan wale walioajiriwa maeneo ya vijijini ili waweze kuanza maisha na kuwatumikia watanzania bila vikwazo vya kiuchumi…
Makamu mwenyekiti wa bodi Husein Kamote alisema mfuko huo unakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha utekelezaji wa mipango yake ikiwemo deni inalolidai serikali ambalo halijalipwa kwa mda mrefu huku likizidi kuongezeka
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akiteta jambo na Mkurugenzi mkuu wa mfuko wa pensheni wa LAPF Eliudi Sanga
Wadau katika mkutano
Mdau kutoka benki ya NMB akizungumza katika mkutano huo
Mwandishi wa habari wa star tv Ramadhan Mvungi akifatilia mkutano kwa ukaribu
Waziri wa TAMISEMI George Simbachawene akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera ,Bunge ,Ajira na Walemavu Jenister Mhagama akipokea zawadi ya saa aliyokabidhiwa na mfuko huo
Waziri wa TAMISEMI George Simbachaweneakimkabidhi kaimu mkurugenzi Geita John Muta hundi ya shilingi milioni saba tu baada ya halmashauri hiyo kufanya vizuri na mfuko huo
Wadau wakifatilia mkutano
Wadau kutoka mifuko mingine pia walishiriki mkutano huo
Mnufaika wa LAPF kupitia maisha popote Scolastika Francis kutoka Kilolo ambaye ni mwalimu akitoa ushuhuda jinsi mkopo huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo sasa anamiliki nyumba pamoja na shamba mbali na ajira yake
Mwalimu wa shule ya sekondari Rombo Njuguna Rombo akitoa ushuhuda jin si mfuko huo ulivyoweza kubadili maisha yake ambapo ameweza kununua
SHARE
No comments:
Post a Comment