Wasichana
wa Shule ya Sekondari Luchelele wakiwa katika picha ya pamoja na
wawezeshaji toka DidaVitengeWear Foundation mara baada ya kupokea taulo
za usafi (Pedi) na Elimu ya Usafi wa mwili na uzazi chini ya mradi wa
Binti Box unaotekelezwa katika shule za Sekondari na Msingi kanda ya
Ziwa.
Kutoka
kulia ni Mkurugenzi wa DidaVitengeWear Foundation ambae pia ni Mratibu
wa Mradi wa Binti Box akijadiliana jambo na Mbunge wa Viti Maalum Vijana
mkoa wa Mwanza kupitia CCM, Mh. Maria Kangoye Ndila (Katikati) pamoja
na Mbunge wa Viti Maalum Wanawake mkoa wa Mwanza Mh. Zawadi Kiteto
(Kushoto), wakati wa utekelezaji wa mradi wa kugawa taulo za usafi kwa
Mabinti wa Shule ya Msingi Igombe.
Mkufunzi
wa Afya ya Uzazi ambae pia ni muuguzi msaidizi kutoka kituo cha Afya cha
Makongoro akitoa elimu ya usafi wa mwili na kuepuka mimba za utoto kwa
wanafunzi wa kike wa shule ya msingi Igombe chini ya mradi wa Binti Box
ulioandaliwa na DidaVitengeWear Foundation kwa kushirikiana na wadau
mbalimbali jijini Mwanza
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Igombe wakiwa katika picha ya pamoja huku wakiwa na
nyuso za furaha baada ya kupewa vifaa vya usafi vitakavyowasaidia katika
mzunguko wao wa kila mwezi na kuepuka magonjwa mbalimbali yanayotokana
na kutumia vifaa visivyo salama.
Kushoto
ni Bi. Khadija Liganga Mkurugenzi wa taasisi ya kusaidia wanawake na
maendeleo ya wasichana yenye makao makuu jijini Mwanza, DidaVitengeWear
Foundation akihimiza jambo juu matumizi mazuri ya vifaa vya usafi kwa
wasichana wa shule ya sekondari ya Bujora (hawapo pichani), Kulia ni
Mbunge wa Viti Maalum Vijana mkoa wa Mwanza, Bi. Maria Kangoye Ndila
ambae aliungana katika mradi huo kuwasaidia mabinti walio shuleni.
Mabinti
wa shule ya sekondari ya Bujora iliyopo Wilayani Magu mkoani Mwanza
wakiwa katika picha ya pamoja baada ya kukabidhiwa taulo za usafi toka
taasisi ya DidaVitengeWear Foundation.
SHARE
No comments:
Post a Comment