
Bunge kujadili hoja ya kumn'goa Zuma Jumanne
Bunge la Afrika kusini litajadili hoja ya kumng'oa rais Jacob Zuma madarakani siku ya Jumanne.
Spika wa
bunge la Afrika Kusini ametoa taarifa hiyo baada ya shinikizo kutoka kwa
vyama vya upinzani vikiongozwa na kile cha Economic Freedom Fighters
(EFF) kinachoongozwa na Julius Malema.
Spika
Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi
rais Zuma kufuatia tuhuma za ufisadi ubadhirifu wa mali ya umma na
matumizi mabaya ya madaraka yake.

Spika Baleka Mbete, amesema wakati umewadia wa kujadili wito wa kumfuta kazi rais Zuma
Vyama vya
upinzani vilikuwa vimemtaka ajiuzulu baada ya kupatikana na hatia ya
kutumia madaraka yake vibaya kwa kuidhinisha ukarabati wa makazi yake
licha ya kushauriwa asifanye hivyo.
Siku ya
Alhamisi, mahakama kuu ya nchi, ilisema kuwa rais amekwenda kinyume na
katiba, katika kashfa ya mamilioni ya dola, yaliyotumiwa kukarabati
nyumba yake ya binafsi.
Upinzani
uliwasilisha kesi mahakamani baada ya bwana Zuma kupuuza uamuzi wa mwaka
2014 kuwa alinufaika kutokana na ukarabati wa nyumba yake na kwamba
alistahili kulipa pesa zilizotumiwa.

Economic Freedom Fighters (EFF) kinachoongozwa na Julius Malema kimekuwa kikimshinikiza ajiuzulu
Mahakama ilisema wizara ya fedha itatambua ni kiasi gani cha pesa kilichotumiwa na kwamba Zuma atatakikana kuzirejesha.
Rais
Jacob Zuma alikubali uamuzi wa mahakama ya kikatiba uliompata na hatia
na akaapa kulipia ukarabati uliofanyiwa makao hayo ya Nkandla kama
ilivyoamua mahakama.BBC
SHARE








No comments:
Post a Comment