
Marehemu Henry Kiherile enzi za uhai wake
Jioni ya
juzi Jumamosi (16/04) Jumuiya ya Watanzania waishio katika jiji la
Houston na miji mingine ya karibu ilifanya Ibada Takatifu katika kanisa
la Umoja kumuaga mpendwa wao Henry Kiherile aliyefariki wiki moja na
nusu iliyopita baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana. Ibada hiyo
ilihudhuriwa na idadi kubwa ya watu waliokuwa na huzuni kubwa juu ya
kifo hicho kilichogusa mioyo ya watu wengi. Mwili wa marehemu Henry
unatarajiwa kusafirishwa kuelekea nyumbani Tanzania kwa
mazishi yanayotarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam siku ya Ijumaa
tarehe 22/04/2016. Pata picha za Misa hiyo hapa chini.
Gari lililobeba mwili wa Henry likiingia kanisani
Wachungaji wakiwa nje ya kanisa kabla ya ibada
Jeneza lililobeba mwili wa Henry likiingizwa kanisani
Dada Lulu ( mdogo wa Marehemu Henry ) akimuaga kwa uchungu kaka yake
Mr. & Mrs. Tenende ( Baba na Mama mkubwa wa marehemu ) wakiwa kanisani. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment