
Papa Francis amekataa kutambua ndoa za wapenzi wa jinsia mojaKiongozi wa kanisa katoliki duniani
Papa
Francis amechapisha mwongozo mpya kuhusu maisha ya familia ambapo
anahimiza kanisa litambue zaidi uhalisia wa maisha ya siku hizi.
Mwongozo
huo ume kwenye waraka aliouandika akizingatia majadiliano ya mikutano
miwili ya wakuu wa kanisa hilo kuhusu sera, maarufu kama sinodi.
Waraka huo ulisubiriwa sana na waumini takriban 1.3 bilioni wa kanisa hilo duniani.
Kicha cha
waraka huo ni "On Love in the Family" (Kuhusu Upendo katika Familia) na
haubadilishi mafundisho ya kidini ya kanisa hilo.
Lakini
unafungua njia kwa maaskofu katika kila nchi kufafanua mafundisho ya
kidini ya kanisa hilo kuambatana na utamaduni wa maeneo yao, mwandishi
wa BBC anayeangazia masuala ya kidini Caroline Wyatt anasema.
Papa
Francis amewahimiza mapadri kutumia hekima na busara wakishughulikia
“familia zilizoumizwa” na kuwa na huruma badala ya kutoa hukumu haraka.
Amekosoa
ubinafsi ambao anasema umewafanya watu wengi katika nchi za magharibi
kuthamini sana kutosheleza mahitaji yao binafsi badala ya mahitaji ya
wake au waume zao katika ndoa.
Huku akiunga mkono kutolewa kwa elimu kuhusu ngono, amesema inafaa kuwa kwenye mfumo wa kutoa elimu kuhusu upendo.
Amesisitiza
sana kuhusu ulezi wa kiroho na kuandaliwa vyema kwa watu kabla ya
kufunganishwa kwenye ndoa kuhusu mahitaji ya maisha katika ndoa.
- Papa Francis awaomba radhi Waprotestanti
- Kwa Picha: Maisha ya Papa Francis
Kadhalika,
amesisitiza kuhusu umuhimu wa mapadri kwenye parokia pamoja na watu
wengine kuwaelewa vyema watu wengine na udhaifu wa binadamu.
Waraka huo ni matokeo ya kazi ya miaka mitatu.

Papa Francis amekuwa akisifiwa kwa unyenyekevu wake na kutetea watu wanaobaguliwa
Papa Francis alituma hojaji kwa familia maeneo mbalimbali ya dunia akiwaomba wamjulishe matumaini yao na wasiwasi wao.
Baadaye, aliwaita maaskofu na makadinali kwa mikutano miwili ya sera za kanisa mjini Roma.
Kwenye
mkutano huo, aliwahimiza kujadiliana na hata kutofautiana kuhusu masuala
ambayo hugawanya waumini wa kanisa hilo katika nchi nyingi.
Masuala
hayo ni pamoja na kutoa komunyo kwa watu waliopewa talaka na wale
walioolewa tena, njia za kupanga uzazi na pia Wakatoliki ambao ni
wapenzi wa jinsia moja.
Ingawa
bado ametoa wito kwa kanisa hilo kutowafungia nje wapenzi wa jinsia
moja, waraka huo haujabadilisha msimamo wa kanisa Katoliki kuhusu
familia za wapenzi wa jinsia moja.
Amehimiza
ushauri wa kidini wa heshima kwa watu hao, jambo ambalo halijakaribia
kutambua familia za watu wa jinsia moja au ndoa za wapenzi wa jinsia
moja kama walivyotaka watetezi wa haki za watu hao.
Waraka
huo, ambao kirasmi hujulikana kama ujumbe wa papa kwa waumini umekuwa
ukivuma sana mtandao wa kijamii wa Twitter kote duniani, wengi wakitumia
kitambulisha mada cha jina lake la Kilatini, #AmorisLaetitia. BBC
SHARE
No comments:
Post a Comment