
Juhudi za
kimataifa za kuumaliza mzozo nchini Libya na kuundwa kwa serikali ya
umoja wa kitaifa zimepata msukumo mpya baada ya serikali iliyokuwa
imejitangazia madaraka mjini Tripoli kutangaza kuachia mamlaka
Hayo
yanakuja ikiwa ni chini ya wiki moja baada ya kuwasili mjini humo,
viongozi wa serikali ya umoja wa kitaifa. Hata hivyo ilikuwa haijawa
wazi kama taarifa yake hiyo ya maandishi ilikuwa inaungwa mkono na
mawaziri wote wa serikali hiyo ya uwokozi. Hatua hii inachukuliwa kama
moja ya hatua za kuipa nafasi serikali ya umoja wa kitaifa kuwa na
mamlaka kamili baada ya miaka kadhaa ya kuwapo na tawala mbili hasimu.
Mataifa
ya magharibi yameonesha imani kwa serikali hiyo inayoungwa mkono na
Umoja wa Mataifa kuwa itasaidia kudhibiti kitisho kinachoasababishwa na
wanamgambo wa kundi la Dola la Kiisilamu nchini humo, kuzuia wahamiaji
ambao wanatumia njia ya Mediterrania kuvuka na kuingia barani Ulaya na
pia kufufua uchumi wa nchi hiyo kwa kuimarisha sekta ya uzalishaji wa
mafuta.
Viongozi
wa serikali hiyo ya Umoja wa kitaifa waliwasili kwa njia ya meli
wakitokea nchini Tunisia jumatanoiliyopita, baada ya serikali hiyo ya
uwokozi iliyokuwa imejitangazia madaraka kufunga anga ya Tripoli ili
kuwazuia wajumbe wa serikali hiyo ya umoja wa kitaifa wasiweze kutumia
usafiri wa ndege kuingia katika mji wa Tripoli.
Kwa
mujibu wa afisa mmoja wa wizara ya sheria nchini humo, taarifa ya
serikali hiyo ya uwokozi imekuja mnamo wakati mawaziri wakikutana kwa
ajili ya kuandaa utaratibu wa kukabidhiana madaraka kwa njia za amani.
Afisa huyo alisema taarifa hiyo ilikuwa na muhuri wa serikali ingawa
haikuwa na jina au saini ya mawaziri.
"Taarifa
hiyo ilisema " kutokana na imani tuliyo nayo katika kuupa umuhimu
kipaumbele cha taifa na pia kuokoa damu ya Walibya tunachukua nafasi hii
kukuarifu kuwa tumeamua kujivua madaraka tuliyo nayo ambayo ni pamoja
na madaraaka ya Rais, mawaziri na manaibu waziri wa serikali
iliyokuwepo" ilisema taarifa hiyo.
Taarifa
za kujiuzulu kwa serikali hiyo ya uwokozi nchini Libya zimepongezwa na
mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika mgogoro huo wa Libya Martin
Kobler ambaye saa chache kabla alikuwa mjini Tripoli kwa ajili ya
kukutana na Fayez Serraj, ambaye ni kiongozi wa baraza linaloungwa mkono
na Umoja wa Mataifa ambalo lina jukumu kubwa la kusimamia ustawi wa
serikali hiyo ya umoja wa kitaifa. Aidha akizungumza na maafisa serikali
hiyo ya umoja wa kitaifa nchini humon mjumbe huyo maalum wa Umoja wa
Mataifa alisema:
Serikali
hiyo ya uwokozi nchini Libya ilishika madaraka baada ya muungano wa
makundi yenye silaha kushinda mapambano kwa ajili ya udhibiti wa mji wa
Tripoli mnamo mwaka 2014 na kuunda bunge lililojulikana kama Baraza kuu
la kitaifa GNC. Bunge na serikali ambayo inaungwa mkono na jumuiya
yakimataifa ilihamia upande wa mashariki mwa Libya. DW
SHARE
No comments:
Post a Comment