
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiongea na
viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania waliomtembelea ofisini
kwake jana jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya
viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania wakimsikiliza Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene jana jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia) akiteta
jambo na viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jana jijini Dar
es Salaam.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene (kulia)
akimsikiliza Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania (JWT) Bw.
Johnsen Estomih Minja mara baada ya kikao chao ljana jijini Dar es
Salaam.

Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene akiwa katika picha
ya pamoja na Viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania jana
jijini Dar es Salaam.
Waziri wa
Nchi Ofisi ya Rais Tamisemi Mhe. George Simbachawene amekutana na
viongozi wa Jumuiya ya Wafanyabiashara Tanzania na kupata nafasi ya
kusikiliza kero mbalimbali zinazowakabili na kuahidi kushirikiana nao
katika kutatua kero hizo.
Akizungumza
na wafanyabiashara hao waliomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar es
Salaam katika ukumbi wa Ofisi ya Rais-Tamisemi wamejadiliana masuala
mbalimbali ya kibiashara ili yaweze kunufaisha jamii na taifa.
“Nimesikia
mapendekezo yenu nitayafanyia kazi, nitawaita ili tujadiliane katika
kujenga mazingira bora na rafiki ya biashara yatakuwa na manufaa kwenu
taifa kwa ujumla” alisema Mhe. Simbachawene.
Serikali
ya Awamu ya Tano imedhamiria kwa dhati kushirikiana na wafanyabiashara
nchini na kulihakikishia taifa kuwa uchumi imara kulingana na Dira ya
Maendeleo ya Taifa ya mwaka 2025.
Katika
kikao hicho wafanyabiashara walipata nafasi ya kumueleza Mhe. Waziri
kero mbalimbali zinazowakabili zikiwepo utitiri wa kodi, ugumu katika
upatikanaji wa leseni na kukosekana kwa uwiano wa tozo za leseni kati ya
sehemu moja na nyingine ambapo Mhe. Waziri aliahidi kufanyia kazi kero
na mapendekezo mbalimbali ya kuboresha mazingira ya ufanyaji biashara
waliyowasilisha kwake.
Akizungumza
katika kikao hicho Mwenyekiti wa Jumuia ya Wafanyabiashara Tanzania
(JWT) Bw. Johnsen Estomih Minja alisema wafanyabiashara wanapenda kuona
Tanzania ikikua kiuchumi na wao kama wafanyabiashara wangependa kuwa
wadau wa kuisaidia nchi kukua kiuchumi, hivyo wanaomba serikali iweze
kuwashirikisha katika masuala mbalimbali yanayohusiana na masuala ya
kibiashara ili waweze kutoa mchango wao wa mawazo na kuondoa ugomvi kati
ya wafanyabiashara na Serikali yao.
Miongoni
mwa masuala ambayo Jumuia ya Wafanyabishara Tanzania imependekeza
yaangaliwe kwa undani kuwa ni pamoja na serikali kuangalia upanuzi wa
wigo wa ulipaji wa kodi,kuunganishwa kwa kodi na tozo mbalimbali katika
ulipaji na kurahisishwa kwa utaratibu wa ulipaji wa leseni. (P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment