
Jeshi la
Misri limepata mabaki ya ndege hiyo kilomita 290 kaskazini ya Cairo.
Baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwemo ndani ya ndege hiyo pia
imepatikana. Kinachotafutwa sasa ni kisanduku cha mawasiliano au "black
box"
Juhudi za
kutafuta kisanduku kinachorekodi mawasiliano au Black box cha ndege
hiyo inaendelea. Ndege hiyo ya Misri ilianguka usiku wa kuamkia Alhamisi
ikiwa na abiria 66 miongoni mwao wahudumu wa ndege hiyo. Shughuli ya
kutafuta mabaki yake ilianza jana na sasa imezaa matunda baada ya
kupatikana kwa mabaki ya ndege hiyo kilomita 290 kutoka Cairo pamoja na
baadhi ya mizigo ya abiria waliokuwemo ndani yake pia imepatikana.
Waziri wa
safari za anga nchini Misri amesema uwezekano kuwa ndege hiyo
ilishambuliwa kigaidi angani ni mkubwa kuliko hitilafu za mitambo
kusababisha kutoweka kwake.
Waziri
mkuu wa Misri Sherif Ismail alipoulizwa uwezekano wa njama ya kigaidi
katika mkasa huo amejibu kuwa hawapuuzilii sababu yoyote inayoweza
kukisiwa kusababisha ndege hiyo kuanguka.
Sababu ya kutoweka ni gani?
Vikosi
vya usalama vya Misri vikishirikiana na vikosi kutoka Ugiriki
vinaendeleza shughuli za kutafuta mabaki zaidi katika bahari ya
Mediterania.
Waziri wa
ulinzi nchini Ugiriki Panos Kammenos amesema ndege hiyo aina ya Airbus
ilifanya mizunguko miwili ya ghafla angani na kushuka ghafla kutoka futi
37,000 hadi futi 15,000 angani, kisha ikatoweka kutoka kwenye mtambo
wao wa rada.
Awali rais wa Ufaransa Francois Hollande alikariri kuwa uchunguzi kamili unahitajika kubaini mkasa huo umesababishwa na nini.
Maafisa
nchini Misri wamesema kuwa ndege ya taifa hilo iliyokuwa ikisafiri
kutoka Paris Ufaransa kuelekea Cairo imetoweka na huenda imeanguka
katika bahari ya Mediterrania. Ndege hiyo ya shirika la EgyptAir ilikuwa
na jumla ya watu 66 miongoni mwao wahudumu wa ndege hiyo. Shughuli za
kutafuta mabaki ya ndege na manusura imeanzishwa.
Ndege
hiyo ilitoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada dakika 45 kabla
ya muda kamili ambao ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Cairo.
Maafisa nchini Misri wanasema ndege hiyo ilianguka mwendo wa saa nane
usiku majira ya Misri, jumla ya saa tatu na nusu tangu kupaa kutoka
uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris. Hii ni muda mfupi
baada ya ndege hiyo kutoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada
maili kumi ndani ya anga ya Misri.
Jamaa za
abiria waliokuwemo ndani ya ndege wamekuwa katika uwanja wa ndege wa
Cairo wakisubiri habari zaidi kuhusu wapendwa wao. Miongoni mwa
waliokuwemo ndani ya ndege hiyo aina ya MS804 ni raia 30 wa Misri,
wafaransa 15, wairaqi 2, watoto wawili na mmoja mdogo, Uingereza,
Kuwait, Ubelgiji, Saudi Arabia, Sudan, Chad, Ureno, Algeria na Canada
wakiwa na raia mmoja mmoja.DW(P.T
SHARE
No comments:
Post a Comment