
Na Tiganya Vincent, Dodoma
Benki ya
Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeiomba Serikali kupitishia fedha
zote za maendeleo katika sekta ya kilimo katika Benki hiyo ili ziweze
kuwafikia walengwa kwa urahisi zaidi.
Kauli
hiyo imetolewa leo mjini Dodoma na Mkurugenzi Mwendeshaji wa TADB Thomas
Samkyi wakati akitoa taarifa yake ya utangulizi kwenye semina ya
wabunge wa Bunge la Jamhuri Muungano wa Tanzania kuhusu kuanzishwa kwa
TADB na majukumu yake.
Alisema
kuwa hatua hiyo itasaidia Benki hiyo kuwa imara ili iweze kutoa huduma
zinazotarajiwa kwa wakulima ambao wengi wako vijijin .
Samkyi
aliongeza kuwa kuimarika kwa Benki hiyo kutaiwezesha kutoa mikopo kwa
wakulima wengi hasa wa vijijini ambao hawawezi kupata mikopo au mitaji
katika Benki za biashara wala kuhimili gharama zake.
Alisema
kuwa mtaji uliopo ni kidogo ambao benki hiyo haiwezi kukopesha miradi
mikubwa wala mikoa mingi kwa muda mrefu kwani itakosa ukwasi katika
kipindi kifupi.
Aida
,Mkurugenzi huyo alisema kuwa pamoja na uhaba wa mtaji TADB imeweza
kutoa elimu kwa wakulima 45,987 ili waweze kupatiwa mikopo.
Naye
Mkurugenzi wa Mipango, Utafiti na Sera wa TADB Francis Assenga Benki
hiyo imeiomba Wizara ya Fedha na Mipango kuweka angalau tengo la
shilingi bilioni 200 katika bajeti ya mwaka ujao wa fedha wakati
taratibu za hati fungamani zikikamilishwa.
Aliongeza kuwa Benki hiyo iliweza kuwekeza sehemu ya mtaji uliopatikana kwenye masoko ya fedha na kupata faida kidogo.
Kwa
upande wa Mkurugenzi wa Mikopo na Biashara wa TADB Robert Pascal alitaja
maeneo 14 ya kipaumbele ya bidhaa za kilimo ambazo zinaweza kupatiwa
mikopo kuwa ni kilimo cha nafaka, kilimo cha mazao ya viwanda(miwa na
korosho) na ufugaji wa ng’ombe.
Maeneo
mengine ni kilimo cha mbogamboga(matunda,mboga mboga na viungo) na
kilimo cha mbegu za mafuta ,kilimo cha mazao ya misitu(ufugaji wa nyuki)
, ufugaji wa kuku wa kienyeji na kuku wa kisasa na ufugaji wa samaki.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment