Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu
Mhe. Dkt Abdallah Possi akizungumza watu wenye ulemavu na wadau wa
maendeleo nchini mara baada ya uzinduzi wa kanzidata kwa ajili ya watu
wenye ulemavu nchini.
Naibu
Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,Kazi,Ajira na Walemavu
Mhe. Dkt Abdallah Possi akifatilia uwasilishwaji wa kanzidata ya watu
wenyes ulemavu nchini iliyotolewa na Ofisi ya Taifa ya Takwimu. Picha na Raymond Mushumbusi MAELEZO.
Na Raymond Mushumbusi – MAELEZO
Bwana
Joachim Marege ni mtu mwenye ulemavu asiyeweza kutembea. Baba huyu
anakofanyia kazi inabidi apande lifti hadi ghorofa ya kumi. Siku moja
nikiwa nimeongozana naye kwenye lifti mara ghafla umeme ukakatika. Baada
ya lift kufunguliwa nikamsaidia kutoka kwenye lift na kuendelea na
safari yangu lakini kwa ndugu huyu haikuwezekana kuendelea na safari
yake kwa kupanda ngazi ilibidi asubiri kwa muda hadi umeme utakaporudi
ndo akapanda lift na kwenda ofisini kwake. Hii ni changamoto sana kwa
watu wenye ulemavu katika kupata miundombinu rafiki ya kuwawezesha
katika shughuli zao za kila siku na ambao idadi yao inaongezeka kila
kukicha.
Mnamo
Aprili 11 2016 Ofisi ya Taifa ya Takwimu wakishirikiana na Ofisi ya
Waziri Mkuu walizindua kanzi data maalum kwa ajili ya kupata takwimu za
watu wenye ulemavu nchini.
Kulingana
na takwimu za Shirika la Afya Duniani, zaidi ya watu bilioni moja dunia
sawa na asilimia 15 ya watu wote duniani wanakadiriwa kuwa na aina
fulani ya ulemavu. Idadi ya watu wenye ulemavu inaongezeka kutokana na
sababu mbalimbali zikiwemo ajali, majanga ya asili na ya kusababishwa na
binadamu, ongezeko la watu hasa wenye umri mkubwa, magonjwa ya
kuambukiza, magonjwa ya akili na matatizo sugu ya kiafya.
Kuongezeka
huku kwa idadi ya watu wenye ulemavu, kunasababisha mahitaji makubwa ya
huduma muhimu za kijamii. Aidha, maisha ya watu wenye ulemavu yanakuwa
magumu zaidi kutokana na unanyanyapaa kutoka kwa jamii kwa ujumla, hali
ambayo inahitaji mabadiliko ya kimtazamo. Ni ukweli ulio wazi kwamba
watu wenye ulemavu hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania wana
matatizo ya upatikanaji wa huduma za kijamii kama vile elimu na afya
ikilinganishwa na watu ambao hawana ulemavu.
Kulingana
na takwimu za Shirika la Afya Duniani (WHO), karibu asilimia 80 ya watu
wenye ulemavu wanaishi katika nchi zinazoendelea. Umaskini hupunguza
uwezekano wa watu wenye ulemavu kupata huduma za kijamii na haki
nyingine za kimsingi. Kwa bahati mbaya programu nyingi za maendeleo
zimeshindwa kuzingatia mahitaji maalum ya watu wenye ulemavu kinyume na
makubaliano ya kimataifa yanayosisitiza uzingatiaji huo kwa ajili ya
maendeleo endelevu.
Tumeshuhudia
majengo yaliyojengwa muda mrefu hata yanayojengwa sasa mengi
hayazingatii mahitaji maalum kwa watu wenye ulemavu. Inabidi katika
ujenzi miundombinu rafiki kwa wenye ulemevu iwekwe ili kuwapunguzia adha
katika maisha watu wenye ulemavu.
Pamoja
na umuhimu na uelewa uliopo bado upatikanaji wa takwimu sahihi ni
tatizo hasa katika nchi zinazoendelea kama Tanzania. Kwenye ngazi ya
kimataifa, bado kuna tofauti kuhusu nini hasa maana ya ulemavu, suala
ambalo husababisha ulinganifu wa takwimu kuwa mgumu. Katika ngazi ya
kitaifa, taarifa za watu wenye ulemavu hazitoshelezi mahitaji ya kuweka
misingi madhubuti ya kupanga na kutekeleza programu za maendeleo
zinazolenga kuboresha maisha ya watu wenye ulemavu.(P.T)
SHARE
No comments:
Post a Comment