TRA

TRA

Saturday, May 21, 2016

WAZIRI MKUU AFAFANUA KUHUSU KUTENGULIWA KWA UTEUZI WA WAZIRI KITWANGA

Share On Facebook ! Tweet This ! Share On Google Plus ! Pin It ! Share On Tumblr ! Share On Reddit ! Share On Linkedin ! Share On StumbleUpon !


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.
“Zipo sheria za utumishi ambazo mtumishi hatakiwi kunywa pombe na wala hapaswi kulewa akiwa kazini... mtumishi anapaswa kuwa na akili timamu inayokuwezesha kufanya kazi za Serikali,” alisema.
Ametoa ufafanuzi leo usiku (Ijumaa, Mei 20, 2016) wakati akijibu swali la mwandishi wa TBC1 aliyetaka kujua kama taarifa zilizoenea kuhusu kutenguliwa kwa Waziri huyo ni za kweli.
“Ni kweli Mheshimiwa Rais, Dk. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016 baada ya kuonekana amelewa wakati wa kazi. Na hili lilibainika pale alipokuwa akijibu maswali ya wizara yake leo asubuhi,” alisema Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu amesema kuna swali aliloulizwa ambalo hakulijibu vizuri na kwamba swali hilo litapaswa kurudiwa kuulizwa baada ya wabunge kuomba muongozo wa swali hilo.
IMETOLEWA NA: OFISI YA WAZIRI MKUU,
L. P. 980,
DODOMA.
IJUMAA, MEI 20, 2016.(P.T)

Author:

«
Next
Newer Post
»
Previous
Older Post

No comments:

Post a Comment

 
Copyright ©2016 NCHI YANGU • All Rights Reserved.
Template Design by AT Creatives • Powered by Blogger