Meneja
Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(katikati)akiongea na
waandishi wa habari jijini Dar es Salam leo(hawapo pichani)wakati wa
Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’itakayowawezesha wateja wa
mtandao huo kujishindia pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi
100.Ili mteja aweze kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma
neno “GO”kwenda namba 15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja
kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu
maswali,Kushoto ni Mkuu wa kitengo cha huduma za ziada wa kampuni
hiyo,Saurabh Jaiswal na Meneja wa huduma za ziada,Mathew Kampambe.
Mkuu
wa kitengo cha huduma za ziada wa Vodacom Tanzania,Saurabh
Jaiswal(kushoto)na Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo,Matina
Nkurlu,wakimsikiliza Meneja wa huduma za ziada wa kampuni hiyo,Mathew
Kampambe(kulia)akifafanua jambo kwa waandishi wa habari(hawapo
pichani)kuhusiana na Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini
Dar es Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia
pesa taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze
kushiriki katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba
15544 aidha mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma
neon”WIN”kwenda namba 15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
Baadhi
ya waandishi wa habari na wafanyakazi wa Vodacom Tanzania,wakiwa kwenye
mkutano wa Uzinduzi wa Promosheni ya ‘Kamata Mpunga’ jijini Dar es
Salaam leo itakayowawezesha wateja wa mtandao huo kujishindia pesa
taslimu kuanzia shilingi Milioni 1 hadi 100.Ili mteja aweze kushiriki
katika promosheni hii anatakiwa kutuma neno “GO”kwenda namba 15544 aidha
mteja anaweza kujiunga moja kwa moja kwa kutuma neon”WIN”kwenda namba
15544 na mteja atapata ujumbe wa kujibu maswali.
Vodacom
Tanzania leo imezindua promosheni kubwa itakayowawezesha wateja wake
kujishindia pesa taslimu kiasi cha shilingi Milioni 615 ndani ya siku
140.Promosheni hii inayojulikana kama ‘Kamata Mpunga’ ni mwendelezo wa
moja ya malengo ya kampuni hiyo ya kubadilisha maisha ya wateja wake
kuwa bora.
Kampuni
hiyo imekuwa ikiendesha promosheni mbalimbali za kubadilisha maisha ya
wateja na watanzania kwa ujumla kama vile Mwaka jana iliendesha
promosheni kubwa ambayo haijawahi kutokea nchini iliyojulikana kama
Jaymillions ambayo ilibadilisha maisha ya wateja mbalimbali walioibuka
washindi na maisha yao kuwa murua. Vilevile miaka ya nyuma kampuni
iliwahi kuendesha promosheni kabambe kama vile timka na bodaboda na
kampeni ya Mahela iliyomfanya Mwanafunzi wa Chuo cha elimu mkoani Kigoma
kuibuka mshindi wa kitita cha shilingi Milioni 100/=.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini leo,Meneja Uhusiano wa Vodacom
Tanzania,Matina Nkurlu amesema promosheni hii inajulikana kama ‘Kamata
Mpunga’ inawahusisha wateja wote wa kampuni yetu na itawawezesha wateja
watakaobahatika kushinda kuwa mamilionea, “kiasi kikubwa cha fedha
kitatolewa kila siku,kila wiki,kila mwezi na pia itakuwepo zawadi kubwa
mwishoni mwa promosheni hii ni rahisi kabisa kila mtu kushiriki.”
Nkurlu
alisema kuwa kila siku kuanzia Jumatatu hadi Jumamosi kutakuwepo na
washindi 3 wa shilingi Milioni 1/= kila mmoja na kila siku ya Jumapili
atakuwepo mshindi wa Milioni 5/= na tarehe ya mwisho wa mwezi katika
kipindi cha promosheni atakuwepo mshindi wa milioni 20/= na kuna mshindi
wa zawadi kubwa ya promosheni ambaye atajinyakulia kitita cha Milioni
100/= ambazo zitatolewa katika kipindi cha mwisho cha promosheni.
Nkurlu
amesema ushiriki wa promosheni hii utakuwa ni rahisi ambapo mteja
anachotakiwa kufanya ni kutuma ujumbe mfupi wa maneno kwa kuandika neno
“GO” kwenda namba 15544 ambapo atapata ujumbe wa kumfahamisha kuwa
ameingia kwenye mchezo na ataanza kupokea maswali atakayotakiwa kuyajibu
kwa ajili ya kujiongezea pointi za ushindi na mteja atakatwa shilingi
300 tu kwenye muda wake wa maongezi ”. Alisema.
Nkurlu
alifafanua kuwa maswali atakayopokea mteja yatakuwa na majibu 2 moja
likiwa jibu sahihi na lingine likiwa sio sahihi. Kila mteja atakapokuwa
anajibu atakuwa anafahamishwa iwapo amepata swali na ataweza
kujipatia pointi. Aliongeza kuwa kila ujumbe utakaotumwa kwenda namba
15544 mshiriki atajipatia bonasi ya pointi 100 za kuanzia ambazo
zitaongezeka kadri atakavyokuwa anajibu maswali.
Nkurlu
alifafanua zaidi kuwa katika ushiriki wa kawaida kwenye promosheni hii
mteja ataweza kujishindia pointi 20 kwa kila jibu la swali litakapokuwa
sahihi na pointi 10 iwapo jibu lake sio sahihi. Pia kutakuwa na bonasi
ambayo itatolewa kwa nusu saa hadi siku nzima kwa lengo la kuwawezesha
wateja wengi kushiriki na kuwa na nafasi ya kujishindia zawadi ya
mamilioni ya fedha. Alifafanua zaidi kuwa kutakuwa na nafasi ya
ushiriki kwa kujiunga moja kwa moja ambapo mteja atatakiwa kutuma neno
“WIN” kwenda namba 15544 na atakakwa kiasi cha shilingi 200 tu.
SHARE
No comments:
Post a Comment