Mgeni
rasmi wa kongamano la kuchangia damu lililoandaliwa na Tanzania Yemen
Professional Foundation (TYPF), Abdallah Ulega ambaye pia ni Mbunge wa
Jimbo la Mkuranga akizungumza umuhimu wa kila Mtanzania kujitolea damu
ili kuinusuru jamii yake. Picha zote na Mpiga Picha Wetu.
MBUNGE
wa Mkuranga, Mheshimiwa Abdallah Ulega, mwishoni mwa wiki aliongozana
na Balozi wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem, katika tukio la
uchangiaji wa damu lililoandaliwa na Taasisi ya Tanzania Yemen
Professional Foundation (TYPF), lililofanyika katika Ukumbi wa City
Garden, jijini Dar es Salaam. Katika tukio hilo, watu mbalimbali
walishiriki katika uchangiaji damu kama sehemu ya kutatua changamoto ya
upungufu wa damu kwa wenye uhitaji, wakiwamo akina mama wajawazito,
ajali za barabarani na majanga mengine.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania, H.E Jasem Al Najem akitolewa damu katika
tukio la kuchangia damu lililofanyika mwishoni mwa wiki katika Ukumbi wa
City Garden, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
katika uchangiaji huo, Mbunge Ulega alisema kwamba jukumu la kuchangia
damu linamuhusu kila Mtanzania, huku akiwataka watu kujenga mazoea ya
kujitolea damu ili kuondoa upungufu wa damu.
Alisema
kwamba mahitaji ya damu kwa nchi yetu ni makubwa, hivyo amefarijika kwa
kupata mwaliko wa kuwa mgeni rasmi sambamba na kuongoza tukio hilo la
uchangiaji wa damu, akiamini amejitolea jambo la msingi na la lazima.
Mbunge
wa Mkuranga mkoani Pwani, Abdallah Ulega, akizungumza na Balozi wa
Kuwait, Jasem Al Najem wakati wanatoa damu kwenye tukio lililoandaliwa
na TYPF mwishoni mwa wiki.
Balozi
wa Kuwait nchini Tanzania, Jasem Al Najem wakati anapima uzito dakika
chache kabla ya kutoa damu katika tukio lililofanyika mwishoni mwiki.
“Nimefarijika
kwa mwaliko wenu na jinsi nilivyoshiriki juu ya utoaji wa damu
nikiamini kwamba naweza kusaidia wenye uhitaji wanapokuwa Hospitalini
ambapo juu ya damu inayohitajiwa kwa kiasi kikubwa ili kuwanusuru
wagonjwa wetu,” Alisema Ulega na kuwataka TYPF kuelekea jimboni kwake
Mkuranga kwa ajili ya kuandaa matukio ya aina hiyo ili waendeleze juhudi
zao za kuchangia damu.
Naye
Balozi Najem alisema kuchangia damu ni sehemu ya malengo yake binafsi
pamoja na ofisi yake, hivyo yupo tayari kusaidia kwa namna moja ama
nyingine ili kuwasaidia watu wote wenye uhitaji wa damu nchini Tanzania.
“Nimejiwekea
utaratibu wa kujitolea katika jamii yakiwamo haya mambo ya damu, hivyo
pamoja na kuwashukuru waandaaji wa tukio hilo pamoja na mliohudhuria
kuja kutoa damu, naomba niwaambie bado nipo tayari kujitolea wakati
wowote itakapohitajika,” Alisema Balozi Najeem.
Awali
Mtendaji Mkuu msaidizi wa TYPF, Swalehe Jabri, aliwashukuru
waliojumulika nao kutoa damu, akisema wamefanya jambo kubwa linalohitaji
kuungwa mkono na kila Mtanzania mpenda maendeleo, akiamini utaratibu
huo umelenga kuwasaidia wagonjwa wenye uhitaji wa damu kwenye hospitali
nchini.
SHARE
No comments:
Post a Comment