Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,
Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akiagana na Katibu wa Siasa na Uenezi wa mkoa
wa Mbeya na Songwe, ndugu Bashiru Madodi. Wakati alipotembelea ofisi
za CCM za muda za Mkoa huo wa Songwe jana.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,
Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akizungumza jambo wakati alipotembelea ofisi
za muda za Mkoa wa Songwe wakati wa ziara yake hiyo jana.
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla akitoa
maelekezo kuhakikisha boma hilo la chumba cha upasuaji linakamilika
ndani ya miezi minne.
…………………………………………………………………………..
Na Mwandishi Wetu, Songwe.
Mbunge wa Nzega Vijijini ambaye
pia ni Mjumbe wa Halmashahuri Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) Taifa,
Mh. Dk. Hamisi Kigwangalla ambaye ni Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya
Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, ametembelea kujionea maendeleo ya ujenzi
wa Boma la jengo la ofisi za chama hicho kwa Mkoa wa Songwe huku
akichangia kiasi cha shilingi Laki Tano.
Dk. Kigwangalla ambaye yupo
kwenye ziara ya kikazi kwenye Mkoa huo mpya kwa ajili ya kukagua huduma
za Afya ambapo alipata wasaha huo wa kutembelea jengo hilo na kueleza
kuwa Serikali ya awamu ya tano ya CCM, itaendelea kuboresha huduma
bora za afya kama Ilani inavyosema ambapo aliwataka wananchi kuendelea
kumuunga mkono Rais Magufuli katika juhudi zake mbalimbali za kulinda
rasilimali za nchi.
“Rais wetu ameongeza bajeti ya
dawa kwa kiasi kikubwa huku mpango wa kuokoa vifo vya akina Mama
wajawazito na watoto wachanga tukilisimamia kwa nguvu zote.. Hii ni sera
yetu na tuendelee kukiunga mkono chama chetu” alieleza Dk. Kigwangalla
na kisha alichangia kiasi cha Tsh. 500,000, kama mchango wake kwa ajili
ya kuchangia maendeleo ya ujenzi huo wa jengo hilo la CCM Mkoa wa
Songwe.
Mbali na kutembelea ofisi hizo za
CCM, Dk. Kigwangalla alipata wasaha wakukagua Hospitali ya Vwawa na
vituo mbalimbali vya Mkoa huo ikiwemo kituo cha Afya Mbuyuni na Iyula.
Wakati huo huo, Dk. Kigwangalla
amemwagiza Mkurugenzi wa Wilaya ya Mbozi, Eliasey Ngowi kukamilisha
boma la chumba cha upasuaji linalojengwa katika kituo cha Afya Iyula na
ujenzi wake ukamilike ndani ya miezi mine.
“Nakuagiza Mkurugenzi boma ili
la upasuaji likamilike ndani ya miezi mine. Na nitakuja hapa kulizindua
mimi mwenyewe, ukae kwenye vikao vyenu huko na kushirikiana na Mbunge wa
hapa, wananchi na hao wahisani muliowapata na mukamilishe haraka sana”
alieleza Dk. Kigwangalla.
Aidha, alipongeza juhudi za
watumishi wa sekta ya Afya kwa kuendelea kutoa huduma bora huku
akimwagiza Mganga Mkuu wa Mkoa wa Songwe kuhakikisha anakamilisha mifumo
ya maji ndani ya chumba cha upasuaji, Maabara na wodi ya Wazazi kwenye
hospitali hiyo ya Vwawa.
SHARE
No comments:
Post a Comment